Raia wa Pakistan wakiwaombea watoto 140 waliouawa katika shambulizi la kigaidi katika shule moja nchini humo.
Raia nchini Pakistan wanaadhimisha
siku tatu za maombolezo kuwakumbuka zaidi ya watu 140 waliouwawa,karibia
wote wakiwa watoto katika shambulio lililotekelezwa na kundi la
Taliban.
Waziri mkuu Nawaz Shariff ameitisha mkutano wa vyama
vyote vya kisiasa nchini humo kujadili vile watakavyoweza kujibu
shambulizi hilo la Peshawar.Ameelezea shambulizi hilo kuwa janga la kitaifa lililotekelezwa na wakatili.
Mkuu wa jeshi Jenarali Raheel Shariff ameahidi kulipiza kisasi kwa kila tone la damu linalomwagika.
Nchini India ,shule zimenyamaza kwa dakika mbili ili kutoa heshima kwa wale waliouawa.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni