Raia mia moja wa Ethiopia hii leo
wamehukumiwa kifungo cha miezi kumi na mbili gerezani nchini Kenya au
walipe faini ya takriban dola 600
Raia mia moja wa Ethiopia hii leo
wamehukumiwa kifungo cha miezi kumi na mbili gerezani nchini Kenya au
walipe faini ya takriban dola 600 baada ya kupatikana na hatia ya kuwemo
Kenya kinyume na sheria.
Polisi waliwakamata wahamiaji wao haramu siku ya Jumatatu katika mtaa mmoja mjini Nairobi. Maryam Dodo Abdalla anaarifu zaidi.
Wahamiaji
hao haramu walioonekana wachafu na waliodhoofika kwa njaa, walikiri
mashtaka hayo baada ya kusomewa makosa yao mmoja baada ya mwingine na
hakimu Victor Wakhumile mjini Nairobi.
Sasa wanatakiwa kutumikia kifungo hicho au walipe faini waliotozwa, na baadaye watasafirishwa kurudishwa Ethiopia walikotoka.
Kwa kilio, wameielezea mahakama kwamba wamewasili Kenya wakiwa wanaelekea Afrika kusini ambako wameahidiwa kupewa ajira.
Polisi
nchini kenya iliwanasa raia hao mia moja wa Ethiopia, mapema wiki hii
wakiwa wamehifadhiwa katika chumba kimoja kidogo, eneo la Embakasi mjini
Nairobi.
Mkuu wa kitengo maalum cha kuzuia uhalifu nchini, SCPU,
Noah Katumo amesema kwamba waliwakamata baada ya kupata fununu kwamba
kuna wageni wengi waliowasili katika mabasi mawili tofuati kutoka
Ethiopia katika mtaa huo.
Raia mia moja wa Ethiopia hii leo wamehukumiwa
kifungo cha miezi kumi na mbili gerezani nchini Kenya au walipe faini ya
takriban dola 600
Miezi kadhaa ya nyuma,
wahamiaji wengine zaidi ya mia moja kutoka Ethiopia walihukumiwa kwa
makosa kama hayo ya kuwepo Kenya kinyume cha sheria na walihukumiwa
miezi sita gerezani.
Ni wahamiaji wengi haramu wanaovuka mpaka na kuingia Kenya kutoka Ethiopia.
Wengi
huitumia Kenya miongoni mwa nchi nyengine kama pia Tanzania, Msumbiji
Malawi na Zambia kama njia ya kupita kuelekea Afrika kusini.
Kwa
mujibu wa ripoti ya shirika la kimataifa la wahamiaji, IOM, ni wahamiaji
17,000 hadi 20,000 wanaoelekea Afrika kusini kila mwaka.
Asilimia 60 ya idadi hii ni wanaume kutoka Ethiopia wanaohadaiwa kwamba watapata ajira na maisha mazuri.
Katika mahakama hiyo hiyo leo, raia watatu wa Kenya wameshtakiwa kwa makosa ya kuwasafirisha kiharamu raia hao 100 wa Ethiopia.
Hatahivyo
wamekana mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya takriban dola 950 na
kesi yao sasa inatarajiwa kutajwa tena tarehe 11 mwezi Machi.
CHANZO BBC.