Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 13 Februari 2015

MAITI ZA VICHANGA KWENYE JOKOFU


Jokofu 
Maiti za watoto wachanga zipatazo tatu zimekutwa zimehifadhiwa kwenye mfuko mweusi wa plastiki wa kutunzia taka na kisha kuwekwa katika jokofu la familia moja na mwili mwingine ulifunikwa kwa nguo.
Inasemekana vichanga hivyo vinakadiriwa kuwa na umri wa mwezi mmoja,na miili hiyo iligunduliwa na rafiki wa mwenye nyumba walikokutwa vichanga hivyo,ambaye alielekea jiji la Johannesburg kwenye maziko ya mpenzi wake.
Anita King, msaidizi wa ndani alitakiwa na mwajiri wake aifanyie usafi nyumba yake na wao wanaelekea mazikoni,na anita alipokuwa katika utekelezaji wa kazi hiyo,akagundua haruku kali ikiingia puani mwake ikitokea katika jokofu la nyumba hiyo.
Naye akadhani labda nyama imeharibika katika friji hilo,na anaeleza ilikuwa ni harufu kali na nzito,na akahisi pengine hayo yamesababishwa na kukatika kwa umeme nchini humo,hivyo akaamua kulifanyia usafi friji hilo na sehemu ya kugandishia.
 Anita anasema,ndani ya jokofu hilo nikakuta mfuko mkubwa wa plastiki wa kuhifadhia taka.
Na mara nlipoufungua mfuko huo nilikumbana na harufu kali mno na mara ikasambaa katika nyumba yote na hata nje ya nyumba pia.sikuyaamini macho yangu anasema Anita niliona kijimkono na kichwa cha mtoto mchanga.sikuwahi kuona kitu kama hiki maishani mwangu anasema Anita .
Wakati wa msiba wa mpenzi wa mwajiri wake! Wageni walikuwa wakipewa mahitaji ya chakula kutoka katika jokofu hilohilo na masalia ya vyakula yalihifadhiwa katika jokofu hilo.
Hata hivyo majirani wanawaelezea wenye nyumba hiyo mahali ambako maiti hizo zilikutwa kuwa ni wacha Mungu na wapenda watoto.
CHANZO  BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni