Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Ijumaa, 13 Februari 2015

TUTAISHAMBULIA BDF XI YA BOTSWANA.

 
 Kocha wa Klabu ya Yanga,Van de Pluijm
Kocha wa klabu ya Yanga, Mdachi Hans Van de Pluijm amesema kuwa watawashambulia wapinzani wao, BDF XI ya Botswana mwanzo mwisho katika kipindi cha kwanza ili kupata ushindi wa haraka katika mechi yao ya raundi ya kwanza ya kombe la shirikisho (vilabu) barani Afrika.
Pluijm amesema wanahitaji sana ushindi wa nyumbani ili kujiweka vizuri kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayofanyika baada ya wiki mbili mjini Gaborone.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kocha huyo, kuna uwezekano wa nahodha wake, Nadir Haroub “Cannavaro” kutocheza kutokana na kuumia mguu huku mshambuliaji Danny Mrwanda akiwa na matatizo ya kifamilia.
“ Huenda watacheza kama watapata afueni kwa matatizo yanayoyasibu, ila uwepo wao ni kwa asilimia ndogo sana”, alisema kocha huyo.
Amesema Yanga, baada ya mechi ya raundi ya kwanza Dar es Salaam, wataondoka Februari 27 kwenda Gaborone kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa siku mbili baadae ili kupata timu itakayosonga mbele.
Maandalizi ya safari hiyo tayari yameanza na mashabiki wa klabu hiyo kongwe, iliyotimiza miaka 80 Februari 11 mwaka huu baada ya kuanzishwa kwake mwaka 1935, wamepanga kukodi mabasi 5 kwa ajili ya kwenda kuishabikia timu yao kwa gharama ya shilingi 250,000 (wastani wa dola 150) kwa kila mmoja ikiwa kama nauli ya kwenda na kurudi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni