Rais Joseph Kabila wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Upinzani nchini Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo umepokea kwa furaha hatua ya tume ya uchaguzi ya
nchi hiyo kutangaza tarehe ya uchaguzi.
Hapo jana Tume ya Uchaguzi
nchini humo ilitangaza uchaguzi mkuu wa rais na wabunge utafanyika
Novemba 27 mwaka 2016 na kutanguliwa na uchaguzi wa serikali za mitaa
baadae mwaka huu.Kutangazwa kwa tarehe hiyo ya uchaguzi mkuu kunakuja wiki chache baada ya ghasia zilizotokea katika miji kadhaa nchini humo kupinga sheria ya uchuguzi mbayo ingesogeza mbele tarehe uchaguzi.
Upinzani na wanaharakati walipinga sherika hiyo kwa madai ilikuwa ni njama za Rais Joseph kabila kuchelewesha uchaguzi huo ili aendelee kutawala.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni