Shirika la afya duniani limependekeza sindano iwe ikitumika mara moja iliizuie maambukizi ya magonjwa
Shirika la afya duniani WHO linatarajiwa hii leo kuzindua hamasisho ya kupunguza maambukizi yanayosababishwa na sindano chafu.
Sindano chafu zimelaumiwa kwa kusababisha mamilioni ya maambukizi ya virusi vya HIV na Hepatatis kila mwaka.Katika kijiji kimoja nchini Cambodia, zaidi ya watu 270 wanaaminika kupata mambukizi ya virusi vya HIV
vinavyosababisha Ukimwi, kwa sababu mhudumu mmoja wa afya alitumia sindano chafu.
Sasa WHO linashauri kuwa uanzilishi wa sindano moja mpya inayotumiwa kwa mtu mmoja na kutupwa,
inafaa kutumika kote duniani na ufikiapo mwaka wa 2020.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni