Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 23 Februari 2015

WATAKA WANAFUNZI WAFUNZWE SOMO LA NGONO.


Somo la ngono Uingereza 
Shule zote za serikali zikiwemo za msingi na zile za upili nchini Uingereza zitalazimika kufunza somo la ngono na uhusiano SRE ,wabunge wa taifa hilo wamesema katika ripoti yao.
Kamati ya elimu katika bunge la Uingereza ilianzisha uchunguzi baada ya kubainika kuwa zaidi ya thuluthi moja ya shule zilikuwa zikishindwa kutoa mafunzo ya somo hilo kwa aumri unaohitajika.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Graham Sturat amesema kuwa vijana wadogo wana haki ya kupata habari ambazo zitahakikisha usalama wao.
Serikali imesema kuwa itaangazia matokeo ya ripoti hiyo.
 Somo la ngono Uingereza
Mwaka 2013 ripoti ya bunge hilo ilisema kuwa masomo ya kibinafsi,ya kijamii ,afya na elimu ya kiuchumi ambapo somo hilo la ngono limehusishwa yanahitaji kuimarika katika asilimia 40 ya shule.
Wabunge hao wamesema:Hali hii haitakubalika katika masomo mengine licha ya kuwa harakati za serikali kuimarisha masomo hayo ni za kiwango cha chini.
Je,unakubaliana na wazo la bunge la Uingereza kuwafunza watoto wa shule za msingi somo la ngono na uhusiano? Kwa maini yako basi ingia katika mtandao wetu wa faceboo katika bbcswahili.CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni