Mashirika mbali mbali ya kiraia
nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameomba majeshi ya Umoja wa
Mataifa ya kulinda amani nchini humo MUNUSCO kufikiria upya mpango wake
kujiondoa kupambana na kundi la waasi la FDLR.
Hapo jana majeshi
ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Jamuhuri ya kidemokrasia
ya Kongo yalitangaza kujiondoa katika operesheni hiyo kwa kushirikiana
na majeshi ya serikali ya DRC hadi hapo serekali ya Kongo itakapotengua
uteuzi wa majenerali wawili walioteuliwa kuongoza opereshini hiyo.Kwa mujibu wa MUNUSCO majenerali hao wana tuhumiwa kufanya vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni