Bi harusi tayari kwa kuolewa,kapambwa kapambika
Bi harusi mmoja kaskazini mwa nchi
ya India alifanya maamuzi ya papo kwa hapo kuolewa na mmoja wa wageni
waliofika kushereheka naye katika harusi yake baada ya mumewe kuugua
ghafla.
Mwanamke huyo ajulikanaye kama Indra anayetokea Rampur
jimbo la Uttar Pradesh, inaelezwa kuwa sekunde chache kabla ya ndoa ya
wawili hao mume akaanguka kifafa, na hivyo kumlazimu kuondoka harusini
na kwenda kumwona daktari.Bi harusi Indra, alishikwa na hasira ya hali ya juu, kwakuwa mume alimficha juu ya hali yake, naye hakuwahi kujua hata siku moja kuwa , jamaa ana tatizo la kuanguka kifafa.
Indra akatoa ombi lake kuwa anahitaji kuolewa na mmoja wa wana familia ya bwana harusi , ambaye alikuja harusini kusherehekea harusi ya nduguye,na Indra akamtaka achukue nafasi ya nduguye badala yake, jamaa akaona nyota ya jaha imemuangukia, si akakubali !
Ndoa ikafungwa, hali ya bwana harusi wa kwanza mwenye kuanguka kifafa, haijajulikana mpaka harusi ya pili ilipokwisha.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni