Rais wa Urusi,Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema
machafuko Mashariki mwa Ukraine yanaleta wasiwasi wa kuweza kuzuka kwa
vita na mwendelezo wa mzozo.
Akizungumza kupitia televisheni Putin
amesisitiza kuzingatiwa kwa mpango wa Amani ya mashariki mwa Ukraine
uliojadiliwa Minsk na kupitishwa na baraza la usalama la umoja wa
mataifaHata hivyo kwa mara nyingine Rais Putin amekanusha madai ya majeshi yake kushiriki katika mzozo.
Kiongozi huyo pia ameyaraja mataifa ya Urusi, ujerumani na Ufaransa kuma washirka mhimu katika utatuzi wa mgogoro huo na kwamba kupitia makubaliano ya Minsk pekee ndiyo itakuwa njia pekee ya kurejesha Amani ya Ukraine.
Kuhusiana na kutuhumiwa kwa taifa lake kuhusika katika mzozo huo Putin amesema wakati mwingine anashtushwa na kauli zinazotolewa na viongozi wa Ukraine dhidi ya Urusi,mfano tuhuma kuwa mamlaka za Urusi zilihusika na machafuko ya viunga vya Maidan mwaka mmoja uliopita.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni