Jumatatu, 23 Februari 2015
MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UGAIDI AUSTRALIA
Wazir mkuu nchini Australia Tonny Abbot ametangaza sheria mpya za kukabiliana na ugaidi.
Hatua hiyo inafuatia kisa cha ugaidi kililichoshuhudiwa majuzi kwenye mkahawa mmoja mjini Sydney miezi miwili iliyopita ambapo watu 2 walipoteza maisha yao.
Bwana Abbot alisema kuwa anapendekeza sheria kuwezesha utawala kufuta uraia wa mtu yeyote mwenyeji wa Australia wanaopigana vita mataifa ya ng'ambo na makundi kama ya Islamic state.
Bwana Abbot pia amesema kuwa kutakuwa na sheria kali za kukabiliana na kile alichokitaja kuwa wale wanaoneza chuki.
Mapendekezo hayo mapya yanakuja miezi miwili bada ya mwanagambo ambaye alidai kuuwa muungaji mkono wa kundi la Islamic state
alipowazuilia mateka 18 wateja wa mkahawa mmoja katikati ya mji wa Sydney akidai kutekeleza mashambulizi hayo kwa niaba ya kundi la wapiganaji wa Islamic state.
Mateka wawili na mwanamme huyo waliuawa wakati polis walipovamia mkahawa huo.
Mtekaji nyara huyo alikuwa ni mhamiaji kutoka Iran.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Habari wa BBC aliyeko Australia ,ushawishi wa waziri mkuu huyo unazidi kudidimia
kwa hivyo hatua hii itamsaidia kujiweka katika ndimi na nyoyo za raiya wa Australia ambao sasa wameanza kukumbwa
na hofu ya kuteikelezwa mashambulizi yanayochangiwa na makundi ya Waislamu wenye msimamo mkali ya kidini.
chanzo bbc.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni