Sadio Mane anayechezea Southampton
Meneja wa Southampton Ronald Koeman
ametoboa siri kuwa jana alilazimika kumwondoa Sadio Mane ambaye ni raia
wa Senegal kwenye orodha ya wachezaji watakaonza katika mechi dhidi ya
Liverpool kwa kosa la mchezaji huyo kuchelewa kuingia uwanjani.
Koeman
amesema ilibidi kumweka mchezaji huyo pembeni na kumpanga mchezaji
aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Benifica Philip Jurisichi kuchukua
nafasi yake.Koeman alisisitiza kuwa timu hiyo imejiwekea kanuni ambazo ni lazima kila mtu azifuate .
Katika mechi hiyo Southampton wakiwa nyumbani walipata kichapo cha magoli mawili kwa bila majibu kutoka kwa Liverpool katika mechi ya lidi kuu ya England.
Hata hivyo Koeman amejitetea kwamba pamoja na kipigo hicho cha jana bado ana matumaini kuwa timu yake itamaliza msimu wa ligi hiyo ikiwa katika nafasi nne za juu za msimamo wa ligi.
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni