Mapigano makali yameendelea
mashariki mwa Ukraine kufuatia majeshi ya serikali kukabiliana na kundi
la Waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Urusi.
Raia wanane na
wanajeshi wanne wameuawa kufuatia mashambulizi ya silaha kati ya majeshi
ya serikali na Waasi katika mji wa Kramatorsk unaoshikiliwa na
serikali.Hata hivyo mapigano hayo yanakuja huku kukiwa na mpango wa mazungumzo ya amani ili kusitisha mapigano hayo. Vyombo vya habari nchini Urusi vinasema makubaliano ya muda ya kusimamisha mapigano yamefikiwa, japo kuwa hakuna uthibitisho wa serikali. Mapambano bado yanaendelea katika mji wa Debaltseve na wanajeshi wa serikali wa Ukraine wamefanya mashambulizi dhidi ya waasi mashariki mwa Mariupol.
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni