Ufaransa imewapokonywa raia 6 vyeti vyao vya kusafiria kwa hofu kuwa walikuwa wanakusudia kujiunga na makundi ya jihad
Kwa mara ya kwanza serikali ya Ufaransa imewapokonya raia sita wa nchi hiyo hati ya kusafiria baada ya madai
kuwa walikuwa wakipanga kusafiri hadi Syria kujiunga na makundi ya itikadi kali ya kidini-Jihad.Usafiri huo ulikuwa umepangwa tayari.
Hatua hizo ni sehemu ya sheria mpya kuhusiana na mapambano dhidi ya vitendo vya kigaidi iliyoanza kutumika mwezi Novemba mwaka jana.
Hati hizo za kusafiria pamoja na vitammbulisho vya kitaifa vimetwaliwa kwa kipindi cha miezi sita ijayo.
Lakini inaweza kuombwa tena upya.
Waziri mkuu wa Ufaransa, Manuel Valls, anasema kuwa ilikuwa ikitarajiwa kuwa hati hizo zingetwaliwa kutoka kwa raia hao wa Ufaransa.
Inakisiwa kuwa mwezi uliopita pekee, zaidi ya watu 1,400 wanaoishi Nchini Ufaransa huenda wamejiunga na makundi ya wapiganaji Nchini Syria au Iraq.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni