Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sis
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi
amesema kuna haja majeshi ya muungano wa jumuiya ya kiarabu ya Pan-Arab
kutoa majeshi yao ili kukabiliana na ugaidi.
Amesema kuwa mataifa
kadhaa yametoa majeshi yao kukabiliana na kundi la wapiganaji wa Kiislam
wa Islamic State tangu kuuawa kwa Wakristuhuko nchini Libya. Mataifa
yaliyotoa misaada ya kifedha na kijeshi ni Jordan,Falme za Kiarabu na
Marekani kwa lengo la kuangamiza kundi hilo Syria na Iraq. Akizungumza
kupitia Televishen Sisi amesisitiza misaada ya kifedha kutoka mataifa ya
Saud Arabia ambao walisaidia wakati wa kuuangusha utawala wa aliyekuwa
Rais wa Kiislam wa Mohammed Morsi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni