Washukiwa kadhaa na wapiganaji wa Kisomali, wamerusha makombora hadi katika ikulu ya Rais katika mji mku wa Somalia Mogadishu.
Wakuu wa usalama wanasema kuwa mlinzi mmoja ameuawa katika shambulio hilo.Kundi la wapiganaji wa Al-Shabab limeshambulia mara kadhaa mji huo mkuu kwa mabomu, likijaribu kupindua serikali ya taifa hilo inayoungwa mkono na mataifa mbalimbali duniani.
Ijumaa iliyopita, walipuaji wa kujitolea muhanga waliwaua zaidi ya watu 20 walipolenga mkahawa maarufu mjini Mogadishu Central Hotel ulioko karibu na ikulu ya Rais.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni