Mauaji ya kundi la Islamic State
Dragana Haines mke wa David
Haines,mamlaka zinapaswa kumsaka na kumkamata akiwa hai mtu aliyemuua
mume wake kwa kumchinja baada ya kutekwa na kundi la wapiganaji wa dola
ya kiislam Islamic State wakati akifanya kazi na shirika la misaada la
Uingereza.Mtu aliyemchinja David Haines na wengine tayari amefahamika
kuwa ni Mohamed Emwazi.
Bi.Dragana amesema tangu alipojua kuwa
mmewe David amechinjwa alijipa matumaini moyoni mwake kuwa ipo siku
muuaji huyo atafahamika na hatimaye kukamatwa.Lakini baada ya kupatika
kwa taarifa hizi za muuaji huyo anasema kuwa itakuwa faraja ya pekee kwa
familia za kila aliyeuawa kinyama na wauaji hao, kwa sababu kama
atakutwa amekufa anaona hicho kitakuwa ni kifo cha heshima kwa Mohamed
Emwazi, lakini maombi yake ni kwamba kukamatwa akiwa hai na afe baadaye.Kwa upande wake Barak Barfi ambaye ni msemaji wa familia ya Sotloff iliyopoteza ndugu yao pia, anasema kuwa hawana wasiwasi juu ya kukamatwa kwake muuaji huyo Mohamed Emwazi ama JIHAD JOHN.
"Tuna Imani kubwa sana na nchi ambayo vyombo vyake vya usalama na kiintelijensia vitawakamata watu hawa.Tungependa kwenda kumuangalia muuaji huyu ana kwa ana wakati wa mashtaka yake katika mahakama ya Marekani,na pia kuona akitumikia kifungo chake, katika gereza maalumu ambako ataishi huko pekee yake katika upweke.hiyo ndiyo sheria ya Marekani na hivyo ndivyo nchi yetu inavyoshughulikia matatizo kama haya"amesema Barak.
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni