Kayla Mueller wa Shirika la Misaada raia wa Marekani aliyeuawa na IS
Marekani imethibitisha kuuawa kwa
Kayla Mueller mfanyakazi wa mashirika ya misaada aliyekuwa akishikiliwa
na wapiganaji wa Islamic State IS.
Familia yake imeelezea
kusikitishwa kwake na kifo cha Kayla Mueller na wazazi hao kwa uchungu
wameonyesha barua aliyowaandikia enzi za uhai wake mara baada ya kuwekwa
kuzuizini na IS. Katika salam zake za rambi rambi Rais Barack Obama
amesema msichana huyo amewakilisha vyema taifa lake la Marekani.
Kumekuwa na taarifa mbili tofauti kutokana na kifo hicho kwani wakati
Marekani inasema bila shaka aliuawa, IS wanasema kuwa Kayla Mueller
aliuaawa katika mashambulizi ya anga huko Jordan,Jordan imekanusha madai
hayo.CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni