Wabunge wa upinzani wakitolewa nje ya Bunge na vyombo vya usalama
Bunge la Afrika kusini liligeuka
kuwa uwanja wa vita ambapo wabunge wa upinzani ilifikia hatua ya
kuvutana mashati na maafisa wa usalama na kufanya wabunge wa upinzani wa
chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) wakiongozwa na Julias Malema
kutolewa nje ya ukumbi wa bunge kwa nguvu na baadae wabunge wengine wa
upanzani nao wakatoka nje ya ukumbi.
Sakata hilo lilizuka wakati
Rais wa nchi hio Jacob Zuma alipokuwa akilihutubia taifa na kuulizwa
maswali na wabunge wa chama cha EFF kinachoongozwa na Julius Malema
wakitaka kujua ni lini atarejesha pesa zilizojengea jumba lake la
kifahari la Nkandla.CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni