Mchezaji akiwa mazoezini
Chama cha Kriketi Tanzania (TCA)
kimetaja kikosi cha wachezaji 14 kitakachocheza na Namibia katika moja
ya mechi za ufunguzi za michuano ya kufuzu kucheza kombe la Dunia
mwakani kwa wavulana waliochini ya miaka 19.
Mechi hizo
zitafanyika siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam ambapo mbali na mechi
kati ya wenyeji Tanzania na Namibia itakayochezwa katika viwanja vya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kenya, watacheza na Nigeria (Uwanja
wa Gymkhana) na Uganda watacheza na Botswana (Uwanja wa Annadil
Burhani).Wachezaji wa timu ya Tanzania ni pamoja na nahodha Arshan Jesani, Godluck Andrew, Salum Jumbe, Juma Mohammed, Shafii Kolo, John Ngati na Hamis Said.
Wengine ni Martin Kavuli, Rashid Awadhi, Umang Somanyi, Razaro Festo, Harshened Anant, Suleiman Nassoro, and Raheel Krishna.
Watakuwa chini ya makocha Khalil Rehemtulla na Hamis Abdallah.
Michuano hiyo ni sehemu ya kufuzu kucheza kombe la Dunia litakalofanyika mwakani, Dhaka, Nigeria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni