rais Goodluck Johnathan wa Nigeria
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan
amekana kwamba alishauriwa kuhusu kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais
nchini humo siku ya jumamosi.
Maafisa wa uchaguzi walichukua hatua
hiyo kufuatia ushauri wa wasiwasi wa maafisa wa usalama kuhusu
mashambulizi ya wapiganaji wa Boko Haram kazkazini mashariki alisema.Kucheleweshwa kwa uchaguzi kwa kipindi cha wiki moja sio kitu kikubwa alisema katika rininga ya taifa hilo.
Upinzani unadai kwamba bwana Johnathan alilazimisha uchaguzi huo kucheleweshwa kwa kuwa alikuwa anaogopa kushindwa.
Uchaguzi huo umeahirishwa hadi 28 mwezi machi.
Wachanganuzi wanasema kuwa uchaguzi huo ndio ulio na ushindani mkali tangu uongozi wa kijeshi ulioisha mwaka 1999.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni