Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Alhamisi, 5 Februari 2015

NIGERIA KUMCHAGUA RAIS JUMAMOSI.


Marais wa zamani wa Nigeria
Nigeria inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Rais Jumamosi ijayo.
Uamuzi uliotolewa kushinikiza uchaguzi huo kufanyika ulichukuliwa baada ya mkutano uliodumu kwa saa saba, katika mji mkuu wa nchi hiyo Abuja, kati ya Wagombea, magavana wa majimbo na Tume ya Uchaguzi.
Hakuna vituo vya kupigia kura vitakavyoandaliwa katika maeneo mengi ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, ambako wapiganaji wa Boko Haram wanafanya mashambulizi yao.
Katika mkutano huo pia imeamuliwa kwamba wale wote waliopoteza makaazi yao kutokana na mapigano hayo, wataweza kupiga kura katika maeneo mengine.
Hata hivyo habari zinasema kwamba mambo mengi kwanza yanahitaji kukamilishwa.
Baadhi ya majimbo yanatarajiwa kutangaza siku za mapumziko kutoa nafasi kwa watu kuhakikisha kuwa wapo katika daftari la wapiga kura.
chanzo bbc

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni