Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Alhamisi, 5 Februari 2015

NATO KUONGEZA NGUVU MASHARIKI MWA ULAYA.


Wanajeshi wa NATO wakiwa kwenye Doria
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema kuwa Urusi inaendelea kukiuka Sheria za kimataifa wakati huu mapigano yakiendelea nchini Ukraine.
Kauli hiyo imetolewa wakati Mawaziri wa Ulinzi kutoka jumuia ya NATO walipokutana mjini Brussels kujadili namna ya kuliimarisha Jeshi hilo, hatua ambayo inaelezwa kuwa kubwa tangu baada ya Vita baridi.
Wakati huohuo,Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani,John Kerry anatarajiwa kufanya mazungumzo mjini Kiev wakati ambapo Marekani inafikiria uwezekano wa kupeleka Silaha kuisaidia Ukraine kupambana na Waasi wanaounga mkono Urusi.
Kikosi cha Wanajeshi 5000 kinatarajiwa kutangazwa, na maeneo watakayokuwa,Stoltenberg amesema mabadiliko haya yanatokana na Mazingira ya kiusalama yalivyo kutokana na kile alichokiita ushari wa Urusi.
Nato pia itaweka wazi mipango yake ya kuanzisha Matawi nchini Estonia,Lithuania,Latvia,Poland,Romania na Bulgaria.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni