Mapigano yanayoendelea yameeathiri Wakazi wa Debaltseve
Shirika lijihusishalo na maswala ya
usalama na ushirikiano barani Ulaya,OSCE limesema hali ya Mashariki ya
Ukraine inazidi kuwa mbaya na mashambulizi dhidi ya Raia yanazidi
kuongezeka.
Msemaji wa OSCE,Shirika linafuatilia hali ilivyo
nchini Ukraine amesema silaha zilizopigwa marufku kimataifa zilitumika
juma lililopta katika mji unaoshikiliwa na waasi Luhansk.Amesema mabomu ambayo yalipigwa marufuku kutumika kwenye maeneo ya Watu wengi chini ya Sheria za kimataifa yamesababisha madhara kwa Raia na kuharibu mali zao.
Baadae hii leo, Mkuu wa Shirika la OSCE atahutubia Baraza lake la kudumu, anatarajiwa kutoa wito wa kusitisha mapigano kwa muda katika Mji unaodhibitiwa na Serikali wa Debaltseve ambao mapigano yameongezeka Wiki za hivi karibuni.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni