Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 4 Februari 2015

WANAJESHI WA CHAD, BOKO HARAM,WAPAMBANA


Wanajeshi wa Chad wako nchini Nigeria kupambana na Boko Haram
Kumekuwa na mapigano makali kati ya Vikosi vya Chad na Wanamgambo wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.Msemaji wa Jeshi la Chad amesema vikosi vyake ambavyo ni sehemu jeshi la kimataifa wamepambana na Boko Haram mjini Gamboru, katika eneo la mpaka wa Nigeria na Cameroon.
Taarifa zinasema Wanajeshi tisa wa Chad na takriban wanamgambo wa Boko Haram 200 wameuawa, lakini idadi ya wanamgambo wanaodaiwa kuuawa haijathibitishwa.
Boko haram wamekuwa wakipambana na Vikosi vya Cameroon upande wa pili wa Mpaka, mjini Fotokol nchini humo.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni