Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 2 Februari 2015

RAIS WA NIGERIA ANUSURIKA BOMU


Rais Goodluck Johnathan wa Nigeria akihutubia uma katika kampeni za uchaguzi
Bomu limelipuka kazkazini mwa Nigeria nje ya uwanja mmoja wa soka ambapo rais Goodluck Johnathan alikuwa amehutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi.
Walioshuhudia wanasema kuwa mlipuko huo ulitokea katika eneo moja la kuegesha magari dakika chache tu baada ya rais huyo kuondoka katika uwanja huo uliopo mji wa Gome.
 Goodluck Johnathan
Bwana Johnathan anafanya kampeni za kutaka kuchaguliwa tena katika uchaguzi unaotarajiwa tarehe 14 mwezi Februari,lakini anakabiliwa na changamoto kubwa ya usalama kutoka kwa kundi la Boko Haram huku kundi hilo likiimarisha mashambulizi yake.
Siku ya jumapili watu watano waliuawa na bomu huko Gombe.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni