Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache
Mtandao wa facebook umethibitisha kwamba unafungua huduma yake ya
messenger kwa wajenzi .Habari hizo zilitangazwa na Mark Zuckerberg
katika kongamano la nane la wajenzi lililofanyika mjini San
Fransisco.Zaidi ya programmu 40 mpya zikiwemo habari za hali ya anga
tayari zimeandaliwa kwa huduma hiyo.Mtandao huo wa kijamii pia
ulionyesha programu yake ya video inayomruhusu mtumiaji kusukuma kamera
huku kanda hiyo ikicheza.
CHANZO BBC.
Sheria madhubuti zinapaswa kutungwa ilikuzima matangazo ya kufana ya vyakula vyenye mafuta mengi.
Madaktari wanasema kuwa wazazi wengi hawajui madhara ya afya kwa watoto walionenepa kupita kiasi.
Katika
utafiti huo uliowajumuisha zaidi ya familia 2,976 nchini Uingereza ni
wazazi 4 pekee waliokuwa na shauku kuwa mtoto wao alikuwa amenenepa
kupita kiasi.
Madaktari wenye walikuwa wamewatambua watoto 369 kati yao waliokuwa na kiwango cha juu cha mafuta mwilini.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa watoto walionenepa kupita kiasi sasa wamekuwa kawaida tu majumbani.
Watafiti hao wanaonya kuwa hili ni janga kwa afya ya jamii. Asilimia 31% ya wazazi hawajui kutambua dalili za mtoto aliyenenepa kupita kiasi
Aidha utafiti huo ulielezea
kuwa takriban mtoto mmoja kati ya watano ambao wanaumri wa miaka 6
tayari wanauzito unaozidi kadri kwa asilimia 14%.
Kundi hilo la
watafiti kutoka taasisi ya usafi ya Uingereza ''London School of
Hygiene and Tropical Medicine'' lilizitembela familia 3,000 na
kuwahoji iwapo watoto wao walikuwa ni wanene kupita kiasi wastani ama
webamba?
majibu yao yaliwaduwaza.
Takriban thuluthi moja 31% ya wazazi walidunisha uzani wa watoto wao.
Proffesa Russell Viner, wa chuo cha Afya ya Watoto aliiambia BBC kuwa
wazazi wa kisasa wanamajukumu wengi na hivyo watoto wao hutunzwa na
vijakazi asilimia kubwa ya muda ambao wazazi wako makazini mwao. Sheria madhubuti zinapaswa kutungwa ilikuzima matangazo ya kufana ya vyakula vyenye mafuta mengi.
''Hili ni janga ambalo
linatokota ,madhara yake yataonekana siku za usoni katika njia ya
maradhi mengi tu yanayohusiani na unene'' alisema Professa Viner.
Kwa mujibu wa Dakta Dame Sally Davies, ''Afya ya watoto kwa sasa
imehujumiwa na dhana kuwa japo mtu ni mnene jamii haitambagua kwani watu
wengi duniani ni wanene''
"Nafikiri kwamba itatubidi tuwaelimishe
wazazi kuhusiana na maswala ya afya ya watoto wao na pia kuwaeleza kuwa
wanapaswa kufuatilia kwa karibu unene au sio wa watoto wao''
CHANZO BBC.
Obama kuzuru Kenya Julai
Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa, Rais Barrack Obama atazuru Kenya mwezi Julai mwaka huu, taifa alikozaliwa babake.
Inasemekana
kuwa Bwana Obama, atahudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu
ujasirimali, utakaofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo-Nairobi.
Tangu awe Rais wa Marekani, Barack Obama hajawahi kuzuru taifa hilo la Afrika Mashariki kama Rais. Obama, atahudhuria mkutano mkubwa wa kimataifa kuhusu ujasirimali
Alizuru mataifa kadhaa za Afrika ikiwemo ziara ya taifa jirani Tanzania mnamo mwaka 2013 bila kuzuru Kenya.
Alizuru Kenya akiwa seneta mnamo mwaka 2006.
Bababke Obama alisomea Marekani na hatimaye kurejea Kenya baada ya Obama kuzaliwa.
chanzo bbc.
Muhammadu Buhari, ni Muisilamu, mzaliwa wa Jimbo la Katsina, Nigeria kaskazini.
Alizaliwa mwaka 1942, Buhari alikuwa kiongozi wa saba wa taifa la Nigeria, baina ya mwaka 1983-1985.
Ni jenerali mstaafu aliyepata mafunzo ya kijeshi katika Nigeria, Uingereza, India, na Marekani.
Na
aliwahi pia kushika nyadhifa za ugavana, kamishna wa raslimali ya
mafuta, mwenyekiti wa shirika la umma la mafuta, na pia mwenyekiti wa
Mfuko wa Amana ya Mafuta. Wafuasi wa rais Buhari wakishangilia ushindi huo
Licha ya kushindwa mara katika chaguzi tatu, amerejea kushindania tena urais, dhidi ya rais alo-madarakani Goodluck Jonathan,
Mkristo,
anaye toka eneo la Niger Delta, kusini Nigeria, kwa mara ya pili,
katika uchaguzi wa Machi. Unaonesha kuwa mchuano mkali.
Kuambatana
na mandhari ya kisiasa, Buhari si limbukeni. Kushindwa mwaka 2003 na
tena 2007, alitambia matokeo ya chaguzi hizo mahakamani bila mafanikio. Buhari alimshinda rais anayeondoka Goodluck Jonathan katika uchaguzi ulioshuhudia ushindani mkubwa
Ingawaje, Buhari anazingatiwa kuwa kiongozi mwenye ufuasi mkubwa na heshima nyumbani, hususan katika rubaa za kaskazini Nigeria.
Na hii inatokana na sera zake za kupambana na ufisadi na ukosefu wa nidhamu, wakati alipokuwa mtawala wa kijeshi. Mabango ya Uchaguzi
Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.
Yajulikana
kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi
waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za
kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,
umeme
na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake,
usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala,
je ni wa kijeshi au kidemomkrasi?
CHANZO BBC.
Majina ya maafisa wakuu wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi yamewasilishwa katika mabunge Kenya
chini
Orodha ya majina ya maafisa wakuu wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi imewasilishwa katika mabunge mawili
nchini Kenya huku kukiwa na mjadala mkali kuhusu jinsi orodha hiyo ilivyowasilishwa bungeni.
Kikao cha bunge la senate lilisitishwa kwa muda kuruhusu wabunge kusoma ripoti hiyo.
Katika
bunge la taifa wabunge nao walitaka kuzima mjadala kuhusiana na ripoti
hiyo iliyowasilisha na raia kwa misingi ya kukiuka sheria.
Robert Kiptoo ana maelezo zaidi kutoka Nairobi.
Orodha
hiyo ina majina 175 ya maafisa wakuu serikalini wakiwemo mawaziri,
makatibu wa wizara na maafisa wengine wa taasisi za umma na hata za
kibinfasi. Maafisa hao wa serikali sasa wameshurutishwa kungatuka madarakani
Maafisa hao wa serikali sasa wameshurutishwa kungatuka madarakani kwa muda wa siku sitini ili kuruhusu uchunguzi wa kina.
Orodha
hiyo ambayo wakenya wakisubiri kwa kwa hamu na ghamu hatimaye
ilijadiliwa katika mabunge yote licha ya upinzani kutoka kwa wabunge
kadhaa.
Mjadala mkali uliibuka katika mabunge hayo hadi spika wa
bunge la senate kusitisha kikao kwa muda kuruhusu masenate kusoma ripoti
hiyo ya rais.
Hata hivyo mjadala ulipoanza wabunge wengi
wanaoegemea upande wa serikali waliunga mkono wakisema vita dhidi ya
ufisadi ni sharti viimarishwe.
wabunge wa upinzani nao wakijaribu kupinga mjadala huo, wakidai kuwa sheria haikufuatwa na rais alipowasilisha ripoti hiyo. Wabunge wa upinzani wanajaribu kupinga mjadala huo
Aidha wamesema kuwa ripotio haina sahihi kama inavyohitajika.
Mpinzani
mkuu wa rais Kenyatta na kiongozi wa upinzai, Raila Odinga, akiongea
baada ya kuwasili nchini kenya kutoka uchina siku ya jumapili,
alisema hatua hiyo ya rais ni sawa na ulaghahi dhidi ya wakenya.
Amesema
kutoka na jinsi mfumo wa mahakama upo, ni vigumu sana kwa uchunguzi
dhidi ya maafisa 175 kukamilishwa kwa siku sitini ikizingatiwa
kuwa kuna baadhi ya kesi za ufisadi ambazo zimesalia mahakamani kwa zaidi ya miaka kumi.
chanzo bbc.
Mahakama
ya Malaysia imemkuta na hatia ya mauaji mtu mmoja kwa tuhuma za mauaji
ya wanafunzi wawili wa udaktari kutoka nchini Uingereza.Mauaji hayo
yanadaiwa kufanyika August mwakajana katika kisiwa cha Borneo.
Jaji
wa mahakama hiyo amesema mahakama imeidhishwa na ushahidi dhidi ya
mshitakiwa na kuona anastahili adhabu. Hukumu hiyo inayomkabili Zulkipli
Abdullah anadaiwa kuwaua Neil Dalton na Aidan Brunger.
Kwa mjibu wa hukumu hiyo ya mauaji, Abbdullah atanyongwa hadi kufa.
CHANZO BBC.
Askari akikagua gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na Joan Kagezi
Watu wenye silaha wamemuua mwendesha
mashitaka mkuu katika kesi ya watuhumiwa wa Kiislam wanaotuhumiwa kuua
watu kadha katika mashambulio ya bomu mwaka 2010.
Mwendesha
mashitaka huyo Joan Kagezi ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi mwendesha
mashitaka msaidizi nchini Uganda ameuawa kwa kupigwa risasi na watu
waliokuwa katika pikipiki wakati akiendesha gari kurudi nyumbani mjini
Kampala.
Kesi inayoendelea inawahusu watu kumi na watatu wanaotuhumiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha al-Shabaab.
Wanatuhumiwa
kuua watu zaidi ya sabini wakati wakiangalia Fainali za Kombe la Dunia
za mwaka 2010 katika mgahawa mmoja na katika uwanja wa klabu ya rugby.
Wiki
iliyopita Marekani ilisema ilipata "habari za kuwepo uwezekano wa
shambulio" katika maeneo ya mji ambayo raia wa mataifa ya magharibi
wanakutana.
Serikali ya Uganda imesema Marekani ilionya juu ya uwezekano wa kuwepo kwa mtu anayejitoa mhanga akijaribu kuingia nchini humo.
Msemaji
wa serikali amesema Uganda ilikuwa katika kitisho kwa sababu imechangia
askari wengi katika jeshi la Umoja wa Afrika linalolinda amani nchini
Somalia wakipambana na kundi la al-Shabab ndani ya Somalia.
CHANZO BBC.
Vyombo vya usalama nchini Kenya,
vinawashikilia wasichana watatu akiwamo Mtanzania, kwa kile kunachodaiwa
kutaka kujiunga na kundi la kigaidi la al-Shabaab huko Somalia.
Taarifa
kutoka kwa Kamishna wa Polisi Jimbo la El -Wak, mpakani mwa Kenya na
Somalia, Nelson Marwa amesema Mtanzania aliyekamatwa, alijieleza kuwa ni
mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Afrika, Sudan.
Mtanzania
huyo, Ummul-Khayr Sadir Abdul (19), mwenyeji wa Zanzibar, anatajwa kuwa
kiongozi wa kundi hilo lililopanga kujiunga na al-Shabaab.
Wasichana wengine waliokamatwa pamoja na Ummul-Khayr, ni Maryam Said Aboud na Khadija Abubakar Abdulkadir wote raia wa Kenya.
“Hawa
wasichana watatu, inaaminika kuwa walikuwa wanakwenda Somalia kupata
mafunzo ya kigaidi na baadaye kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga,”
alisema Kamishna Marwa.
Akizungumzia suala hilo, Kaimu Mkurugenzi
wa Makosa ya Jinai, DCI Diwani Athumani alisema: “Tunafuatilia
hatujapokea taarifa zaidi ya hizo.”
Kamishna Marwa alisema raia
hao wawili wa Kenya, mmoja ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya
kilichopo Thika, Jimbo Kiambu na mwingine ni mwanafunzi wa Sekondari ya
Burhania, iliyopo Malindi, Kilifi.
“Serikali imepata taarifa
kuhusu watu wanaokusanya watu kutoka Afrika Mashariki ili wakajiunge na
makundi ya ugaidi nchini Somalia, wakala wetu wa usalama wamepata
taarifa hizo na kufanikisha kukamatwa kwa wasichana hao,” alisema
Kamishana Marwa.
Hivi karibuni, tovuti ya al-Jazeera ilitoa
taarifa za kukamatwa kwa mkanda wa video ulioonyesha mwakilishi wa kundi
la kigaidi la Dola ya Kiislamu ya Iraq na Levant (ISIL) akimtaka
kiongozi wa kundi la al-Shabaab kuliimarisha kwa kufanya mashambulizi ya
kigaidi katika miji ya Mwanza na Dar es Salaam.
Kamishna Marwa
alisema ingawa nyaraka za wasichana hao zote zinaonyesha kuwa ni
wanafunzi, lakini bado walibanwa kwa maswali kuhusu sababu inayowapeleka
nchini Somalia.
Aliongeza zaidi kuwa chanzo cha habari cha
kiusalama kilieleza kuwa nyaraka za wasichana hao zilionyesha kuwa
walikuwa wakienda kuolewa na wanajeshi wa kundi la al-Shabaab.
chanzo bbc.
Jenerali Muhammadu Buhari anaongoza
kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye
ni rais Goodluck Jonathan
Huku yakisalia majimbo machache, Buhari anaongoza kwa karibu kura milioni tatu mbele ya Rais wa sasa Goodluck Jonathan.
Awali
kulikua na matukio ya kurushiana maneno katika ukumbi mkuu wa hesabu ya
kura pale mwakilishi wa chama tawala-PDP Elder Orubebe alipolalamikia
tume ya uchaguzi kwa kupendelea.
Kumekua na kurushiana cheche za maneno makali katika ukumbi mkuu wa kuhesabu kura nchini Nigeria.
Mwakilishi
wa chama tawala PDP-Elder Orubebe, alivuruga shughuli ya kutangazwa
matokeo ya kura akidai tume ya uchaguzi ilikua ikipendelea upande mmoja. Mawakala wa wagombeaji wakuu
Mwenyekiti
wa tume ya kitaifa ya uchaguzi mkuu Nchini Nigeria, Attahiru Jega,
alimuonya Elder Orubebe kuwa mwaangalifu kutokana na matamshi yake hayo
aliyotoa.
Mwandishi wa BBC aliyeko ukumbi huo mjini Abuja anasema huenda vurugu hizo ni ishara kuwa, PDP inahisi kushindwa.
Huku
majimbo mengi yakitoa matokeo yake mgombea wa upinzani, Muhammadu
Buhari wa chama cha APC, anaendelea kuongoza kwa wingi wa kura, huku
akifuatiwa na Rais Goodluck Jonathan.
Generali Buhari wa chama cha
All Progressives Congress (APC) anaonekana kusajili matokeo mema mapema
hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos.
Matokeo ya
uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache
zinazokuja wakati
majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo
yao. Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne Mwandishi wa BBC mjini Abuja amesema mchuano bado ni mkali.
CHANZO BBC.
Brazili jana aliikimbiza mchamchaka Ufaransa baada ya kuichabanga magoli matatu kwa moja.
Haikuwasaidia
Ufaransa kuanza kuona lango la Brazil katika dakika ya 21 kwa goli
lililofungwa na Raphael Varane kwani ni kama waliichokoza kundi la nyuki
kwani goli hilo lilirudishwa na Oscar dos Santos Emboaba Júnior katika
dakika ya 40, na hatimaye kushindiliwa magoli mengine mawili kupitia kwa
Neymar da Silva Santos, Júnior, na Luiz Gustavo na hivyo hadi mechi
hiyo inamalizika Brazil 3 Ufaransa 1.
Katika mechi nyingine za
kimataifa za kirafiki zilizochezwa hapo jana, Bahrain iligeuzuwa chapati
na Colombia pale waliposhindiliwa magoli 6 kwa mtungi huku Iran ikiwapa
darasa Chile kwa kuichabanga magoli mawili kwa nunge.
Leo kutakuwa na mechi moja ya kimataifa ya kirafiki ambapo Canada watairibisha Guatemala
CHANZO BBC.
Nahodha wa kilabu ya Chelsea John Terry ameongeza mkataba wake katika kilabu hiyo hadi mwisho wa msimu wa mwaka 2015-16.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34,ambaye mkataba wake wa awali unakamilika mwisho wa msimu huu ameichezea Chelsea mara 550.
Chelsea
wanaongoza kwa pointi sita katika jedwali la ligi ya Uingereza wakiwa
na mechi moja zaidi ambayo hawajacheza dhidi ya wapinzani wao na
mkufunzi Jose Mourinho anasema kuwa kandarasi hiyo ya mwaka mmoja si ya
kumpatia asante John Terry bali ni kwa sababu anaendelea kucheza vizuri.
Ni mlinzi wa kiwango cha juu.
Mourinho
hivi majuzi alisema kuwa ana hakika kwamba Terry atapewa mkataba
mpya,ikiwa ni miongoni mwa sera za kilabu hiyo kuwaongezea kandarasi
awchezaji ambao wamepitisha umri wa miaka 30.
CHANZO BBC.
Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot
anasema kuwa hajakosana na meneja Arsene Wenger na kuongezea kwamba bado
hajaanza mazungumzo ya mkataba mpya na kilabu hiyo.
Mkataba wa Walcot unakamilika mwaka 2016 na Wenger amesema kuwa anatarajia kuwa na mda mrefu wa makubaliano.
''Ripoti zinazosema nimekosana na kocha juu ya kandarasi ni upuzi mtupu'',alisema mchezaji huyo wa miaka 26.
Hatujaanza mazungumzo yoyote juu ya kandarasi yangu na lengo langu kuu ni kufanya vyema katika kilabu hii.
CHANZO BBC.
Mabondia Xin Hua wa China na Mohamed Matumla wa Tanzania wakitambiana kabla ya pambano lao la Ijumaa
Bondia Mohamed Matumla wa Tanzania atapanda ulingoni Ijumaa kutwangana na Wang Xin Hua wa China.
Mchezo huu ni wa uzito wa super bantam kuwania nafasi ya kugombea taji
la dunia la WBF utakaofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini
Dar es salaam Tanzania.
Mshindi wa mpambano huu wa kukata na
shoka atapata nafasi ya kupanda ulingoni kwenye mpambano wa utangulizi
katika pambano litakalo wakutanisha wababe Floyd Mayweather na Manny
Pacquiao.
Hili litakuwa ni pambano la 17 kwa Mohamed Matumla,
tangu aanze ngumi za kulipwa akiwa ameshinda mara 11, amepoteza mara 4
na kutoka sare mara 2.
Pambano hili litatanguliwa na mapambano
kadhaa ya awali kati ya Ashraf Suleiman wa Tanzania ataonyeshana umwamba
na Joseph Rabotte wa Marekani katika pambano la uzito wa juu.
Kalama Nyarawila na Thomas Mashali, wote wa Tanzania watapambana katika uzito wa kati kuwania taji la WBF.
Huku Japhet Kaseba wakipepetana na Maada Maugo katika uzito wa Light kuwania ubingwa wa taifa.
Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India
Amini usiamini mtoto mwenye umri wa miaka miwili ameweka rekodi ya taifa ya ulengaji shabaha kwa mishale nchini India.
Kulingana na vitabu vya kumbukumbu ya rekodi za taifa, Dolly Shivani Cherukuri kutoka Vijaywada katika jimbo la Andhra Pradesh
aliweka rekodi ya kuwa mshiriki mwenye umri mdogo zaidi kusajili alama 200 katika mashindano yaliyoandaliwa jumanne iliyopita.
Kulingana
na jarida la Press Trust la India ,mtoto huyo alifuma mishale 36
kutoka umbali wa mita 5 na kisha umbali wa mita 7 na kujizolea alama
388.
Tukio hilo lilishuhudiwa na wachezaji wakongwe na maafisa kutoka idara ya kumbukumbu za michezo.
''kwa hakika tunajivunia matokeo haya ''alisema afisa wa shirikisho la mishale la India bwana Gunjan Abrol.
Dolly ambaye alizaliwa baada ya kupandikizwa kwa mbegu ya babake kufuatia kifo cha kakake katika ajali ya barabarani. Mtoto wa miaka 2 aweka rekodi India
Kakake alikuwa mrushaji mishale wa kimataifa Cherukuri Lenin.
Babake Cherukuri Satyanarayana ,anasema kuwa Dolly alifunzwa kufuma mishale, tangu alipozaliwa.
Babake ni mmiliki wa klabu kimoja kinachofunza kurusha mishale.
Aidha aliiambia shrika la habari la AFP kuwa kitambo alikuwa
amemptengezea uta na mishale nyepesi ilikukuza talanta ya mtoto huyo.
Sasa
babake anasema kuwa anapanga kumshirikisha mwanawe katika mashindano
kwa nia ya kumsajili katika vitabu vya rekodi za dunia za Guinness.
CHANZO BBC.
Cambridgeshire
Madaktari wa upasuaji huko
Cambridgeshire wamefanya upandikizaji wa kwanza wa moyo barani Ulaya kwa
kutumia moyo mwengine uliosimama kufanya kazi.
Myoyo hiyo hupatikana kutoka kwa watu waliokufa lakini ambao myoyo yao bado inafanya kazi.
Katika upasuaji huo,moyo huo ulitoka kwa mtu ambaye mapafu yake na moyo wake ulikuwa haufanyi kazi.
Hospitali ya Papworth inasema kuwa mbinu hiyo huenda ikaongeza idadi ya myoyo inayopatikana kwa asilimia 25.
Mgonjwa
aliyewekwa moyo mpya kwa jina Huseyin Ulucan, mwenye umri wa miaka 60,
kutoka London,alikabiliwa na shinikizo la moyo mwaka 2008.
Alisema:kabla ya upasuaji,sikuweza kutembea na nilichoka sana,kwa hakika siku na maisha mazuri. Upandikizaji wa moyo
Lakini anasema kuwa amefurahishwa na kuimarika kwa afya yake tangu upandikizaji huo.
Kwa sasa najisikia mwenye nguvu kila siku,na nimetembea hadi haospitalini asubuhi hii bila tatizo.
Kumekuwa na visa 171 vya upandikizaji wa myoyo katika kipindi cha miaka 12 iliopita nchini Uingereza.
Lakini mahitaji yanashinda myoyo iliopo ,hivyobasi wagonjwa wengine hungoja kwa miaka mitatu kupata kiungo kinachowafaa.
Wengi ya wagonjwa hao hufariki kabla ya kiungo kupatikana.
CHANZO BBC.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima
amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu
dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akiongea kabla ya kuhojiwa na
polisi Mchungaji Gwajima amejitetea kuwa alichofanya ni kutumia fursa ya
kumuonya kiongozi mwenzake wa kiroho kutokana na kuwageuka wenzake
katika makubaliano waliofikia katika tamko la kuipigia kura ya hapana Katiba inayopendekezwa.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kumkadhifu na kumtukana hadharani Kardinali
Pengo. Inadaiwa matusi hayo yameonekana kupitia mitandao mbalimbali ya
kijamii ya WhatsApp na mingineyo, ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na
picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana
kwa maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu
wengine.
CHANZO BBC.
Funza hao walioondolewa puani kama wanavyoonekana.
Mwanamume mmoja amekutwa na
kuondolewa funza wapatao mia moja walio hai tena wanao kula kula puani
mwake na kuruhusiwa aende nyumbani .Mwanamume huyo anatajwa kuwa na umri
wa miaka sitini na mitano ,na watabibu wanasema funza hao walikuwa
wamejichimbia ndani zaidi ya pua yake.
Mwanamume huyo ni mwenye
asili ya Sao Paulo, nchini Brazil,alikuwa akisumbuliwa mno na njia ya
mfumo wa hewa hasa puani ,na pua yake ilikuwa imeathiriwa na mabuu ya
inzi.
Pamoja na mambo mengine, mara kwa mara mwanaume huyo alikuwa
akilalamika kuwa kuna minyoo pia huwa inadondoka kutoka puani mwake.
Tundu za pua ni mahali ambapo vijidudu virukavyo huweza kutaga mayai yao hapo na baadaye hugeuka kuwa funza.
Na
wataalamu wa pua na koo wanasema kwamba chakula kikuu cha funza wakaao
puani ni nyama za pua na endapo mgonjwa ataachwa bila kupatiwa matibabu
,funza hao wanauwezo wa kutafuna na kuharibu kabisa mfupa wa mwanzi wa
pua,kuharibu vimishipa vya uso,pua na macho.
Na hali hiyo
ikitokea,jua kutakuwa na maambukizi kwenye ubongo na macho na kwa
kawaida husababisha ugonjwa wa uti wa mgongo na hata kifo.
Mwanaume
huyo aliamua kwenda kwenye zahanati nchini Brazil kutoa malalamiko yake
kwamba siku mbili nyuma aliona kitu kinachofanana na mnyoo ukichomoza
na hatimaye kutoka katika pua yake upande wa kushoto. Funza wakiwa puani
Mwanaume huyo anaishi na virusi
vya ukimwi ana tatizo la ini,na kinga yake ya mwili ilikuwa inapungua
kwa kasi kubwa na alikuwa hajaanza kutumia vidonge vya kurefusha maisha.
Miaka
mitano iliyopita alifanyiwa upasuaji wa pua yake baada ya kugundulika
kuwa alikuwa na uvimbe puani na hakuona dalili yoyote hapo kabla,ingawa
kwa wiki nzima kabla ya kuhudhuria zahanati alikuwa akitokwa na damu
puani,maumivu ya pua upande wa kushoto
Na harufu mbaya,alikuwa akishindwa kupumua sawa sawa na uvimbe ulianza kuonekana usoni na puani mwake.
Lakini baada ya kudumbukiza kijikamera kidogo puani mwake ,aligundulika
Madaktari wakaanza kuwatoa funza hao kwa muongozo wa kamera iliyokuwa ikiangaza puani na kuitibu pua yake.
Iliwachukua
siku nne madaktari kuondoa uambukizo katika pua ya mwanaume huyo na
baada ya hapo madhila yake yakakoma na baada ya uangalizi wa mwisho kwa
kutumia kamera ile ile imethibitika kwamba tatizo lake lime kwisha.
CHANZO BBC.
Raia wa Sierra Leone waanza kusalia majumbani kwa siku tatu kwa lengo la kukabiliana na ebola
Mamlaka nchini Sierra Leone imeanza
kutekeleza hatua ya kutotoka kwa siku tatu miongoni mwa raia wake
itakayosaidia kukabiliana na kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa wa ebola.
Takriban
watu millioni sita wametakiwa kusalia majumbani mwao kwa kipindi cha
siku tatu huku watu wa kujitolea wakitembelea nyumba hadi nyumba
kuwasaka watu walio na ishara za ugonjwa huo huku wakiwashauri wengine
jinsi ya kuepuka maambukizi.
Visa kadhaa bado vinaendelea kuripotiwa kazkazini na Magharibi mwa Sierra Leone kila wiki.
Mataifa
matatu ya Afrika Magharibi yalioathiriwa vibaya na Ebola Sierra
Leone,Liberia,Guinea-yameweka lengo la kutokuwa na hata kisa kimoja cha
ebola ifikiapo katikati ya mwezi ujao.
CHANZO BBC.
Jeshi la Nigeria linasema kuwa limeuchukua mji wa kazkazini mashariki wa Gwoza unaoaminika kuwa ngome kuu ya Boko Haram.
Ni
katika eneo hilo ambapo wapiganaji wa Boko Haram walitangaza uongozi wa
kiislamu na ni miongoni mwa miji mikuu iliotekwa na kundi hilo katika
kipindi cha hivi karibuni.
Tangazo hilo linajri siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Uchaguzi
huo uliahirishwa kwa mda wa wiki sita ili kutoa fursa kwa jeshi la
muungano wa mataifa kupata mda zaidi wa kukabiliana na Boko Haram.
Rais wa Chad,taifa ambalo ni miongoni mwa yale yaliyo na vikosi vyake amesema kuwa vikosi vya Nigeria havijajizatiti.
CHANZO BBC.
Ajali ya ndege
Viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani wanasema kuwa wamepata ushahidi
unaosema kwamba rubani wa ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya
ALPS na kuwaua abiria 150 alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugonjwa
anaougua.
Maafisa
hao pia wamesema kuwa walipata kijikaratasi cha ugonjwa kilichokuwa
kimekatwa ambacho kilimtaka rubani huyo kupumzika siku ya kuanguka kwa
ndege hiyo. Maafisa wa Polisi wa ujerumani
Hatahivyo hawakupata ujumbe wowote wa rubani huyo kutaka kujitoa uhai wake.
Vyombo
vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kwamba faili ya rubani Andreas
Lubitz mwenye umri wa miaka 27 katika shirika la anga za juu imeonyesha
kuwa Andreas alikuwa na matatizo ya akili na alitakiwa kufanyiwa ukaguzi
wa mara kwa mara. Andreas Lubitz Ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa alilazimika
kuchukua likizo ya miezi sita kutoka kwa mafunzo ya urubani kutokana na
shinikizo la akili.
Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe
Mabibi harusi wa zamani wawili
wameamua kuipeleka serikali ya Zimbabwe mahakamani katika harakati za
kuvunja sheria kandamizi nchini humo na kutaka sheria inayoruhusu
mabinti kuolewa wakingali wadogo iwe ni kinyume na katiba na si halali
kwa kifupi iharamishwe.
Mabibi harusi hao Loveness Mudzuru na
Ruvimbo Tsopodzi wamesema ndoa za utotoni ,ambazo ni ruksa nchini
Zimbabwe,wansema ni sawa na ukatili wa kijinsia kwa watoto ambao
huwanasa mabinti na kuishia katika janga la umasikini na madhila
yasiyosemeka.
Nimekabiliana na changamoto zisizosemeka ,mume wangu
alikuwa akinipiga sana.nilikuwa natamani kuendelea na masomo lakini
yeye alikataa.nilikuwa na hali mbaya sana huu ni ushuhuda wa Tsopodzi,
mama wa mtoto mmoja,mama huyu aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na
mitano tu .
Na anaendelea kusema kwamba anataka kuchukua hatua
hiyo ili kuleta tofauti,ameeleza hayo akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo
Harare mapema wiki hii.Na hii yote ni katika harakati za kuzuia mabinti
wadogo wanaoolewa katika umri mdogo.
Takwimu zilizochapishwa
mwaka wa jana zinaonesha kwamba moja ya tatu ya wasicha walio na umri wa
chini ya miaka kumi na nane huolewa , wakati wengine wapatao asilimia
tano huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka kumi na mitano.
Katika
tamko lao kwa mahakama ya katiba, Tsopodzi na Mudzuru, ambao kwa sasa
wana miaka 19 na mwingine ana miaka 20, wanasema kwamba sheria ya ndoa
nchini Zimbabwe ni ya kibaguzi kwani inamtaka mtoto wa kike aolewe akiwa
na umri wa miaka kumi na sita wakati mtoto wa kiume anatakiwa kuoa
akishatimiza umri wa miaka kumi na nane, na ndoa za kimila hazijaainisha
umri halisi wa kijana ama binti kuoa ama kuolewa.
Sheria ya ndoa
ya mwaka 2013 inasema kwamba kila mtoto mwenye umri wa miaka kumi na
mitatu,anayo haki ya kupata malezi ya wazazi,elimu na ulinzi kutoka kwao
katika masula ya unyonyaji kingono na kiuchumi.
Sheria hii pia
haijaweka wazi umri wa kuoa ama kuolewa lakini inasisitiza kwamba hakuna
mtu yeyote atakayelazimishwa kuoa ama kuolewa kinyume na matakwa yao na
kuonesha wazi kuwa raia wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka kumi na nane
anaweza kuwa na familia yake.
Umasikini ndio chanzo cha ndoa za
utotoni nchini Zimbabwe na kuwasababisha kuolewa kabla ya umri wao
wasichana walio wengi ,na hivyo kuwasababisha wazazi kupunguza mzigo wa
familia katika masuala ya matunzo na kubakisha mama tu na baba.ulipwaji
mahari nayo ni motisha inayowafanya wazazi kutowatendea haki watoto wao.
Baadhi ya familia nchini Zimbabwe zinatukuza ndoa za utotoni kwa mtazamo wa kuwalinda watoto wao wa kike na ngono kabla ya ndoa.
Mudzuru
anatoa ushuhuda wake kwamba ndoa za utotoni ni chagamoto kubwa ,kwani
mabinti hao walio katika umri mdogo watazaa watoto wakiwa katika familia
masikini na hapo ndipo mzunguuko wa ndoa za utotoni unapoanza upya.
Mudzuru,
aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na sita kwa sasa ana watoto wawili
tena akiwa hajatimiza miaka kumi na nane ,anasema maisha yake yalikuwa
sawa na jehanamu ya moto na aliishi maisha yake katika dhiki
isiyosemeka.
Nasema maisha yake yalikuwa magumu sana, kulea watoto
ilhali wewe mwenyewe ukiwa ni mtoto ni vigumu,na asema katika umri wake
alipaswa kuwa anahudhuria masomo shuleni.
Naye mwanasheria wa
mabinti hao ambao ni akina mama sasa hivi,alikuwa ni waziri wa zamani wa
fedha nchini humo Tendai Biti, aliwasilisha changamoto hizo za kisheria
mwezi January mwaka huu.
Beatrice Savadye,yeye ni mwanaharakati
wa kupinga ndoa za utotoni nchini humo anayeongoza asasi isiyokuwa ya
kiserikali,ijulikanayo kaka ROOTS ,asasi ambayo inawaunga mkono akina
mama hao wawili anasema kesi hiyo imekuwa na mvuto wa kipekee nchini
humo nan je ya nchi hiyo kwa ujumla wake.
Na anamashaka kama mahakama itatoa maamuzi yake lini ,lakini inalazimika kutoa maamuzi yake ndani ya miezi sita. Wazimbabwe
Ulimwenguni kwa ujumla wake
wasichana milioni kumi na tano wanaolewa kila mwaka.katika jangwa la
sahara peke yake asilimia arobaini ya wanawake huolewa wakiwa katika
umri mdogo.
chanzo bbc.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Suleimani Msindi ‘Afande sele’, ametangaza
nia ya kuwania ubunge wa Morogoro mjini kupitia Chama cha Alliance for
Change and Transparency (ACT-Tanzania). Msanii huyo ametangaza azma yake
baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama cha Chadema.
Yanga ya Tanzania imeitumia salamu timu ya Platinum FC ya Zimbabwe kufuatia ushindi mfululizo katika ligi kuu ya Tanzania Bara.
Yanga
imeifunga JKT Ruvu 3-1 katika ligi kuu Tanzania Bara, huku Danny
Mrwanda, aliyewahi kucheza soka huko Vietnam akifunga goli moja na Simon
Msuva akitupia mawili katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni, Yanga pia iliwafunga Mgambo Shooting 2-0 ikiwa ni
mfululizo wa ushindi katika mechi zake
Mechi hizo ni sehemu ya
maandalizi kwa safari ya Yanga kuelekea Zimbabwe kurudiana na Platinum
FC katika mechi ya kombe la Shirikisho barani Afrika mapema mwezi ujao.
Yanga
ilishinda 5-1 katika mechi ya awali ikiwa uwanja wa nyumbani na
inahitaji ushindi wa aina yoyote, droo au hata ikifungwa magoli
yasiyozidi 4 ili isonge mbele kunusa hatua ya 16 bora.
Yanga kwa
sasa inaongoza ligi kuu Tanzania Bara ikiwa a pointi 40 katika michezo
19 iliyocheza huku Azam ikifuatia ikiwa na pointi 36 katika michezo 18
iliyocheza.
CHANZO BBC.
Mlinzi wa kilabu ya Liverpool Martin
Skrtel atahudumia marufuku ya mechi tatu baada ya kamati ya nidhamu ya
shirikisho la soka nchini Uingereza FA kukataa ombi lake la kukata rufaa
dhidi ya hatua ya kinidhamu dhidi yake.
Raia huyo wa Slovak
alimkanyaga kipa wa Manchester United David de Gea katika dakika za lala
salama za ushindi wa 2-1 wa Manchester United dhidi ya Liverpool katika
uwanja wa Anfield siku ya jumapili.
Tukio hilo halikuonekana na refa Martin Atkinson.
Skrtel mwenye umri wa miaka 30 alisema kuwa kisa hicho hakikuwa cha makusudi.
Hatahivyo
kamati hiyo ya nidhamu ilikataa ombi hilo hatua ambayo itamfanya
mchezaji huyo kukosa mechi tatu za EPL huko Arsenal,Newcastle, pamoja na
robo fainali ya kombe la FA dhidi ya Blackburn.
CHANZO BBC
Serikali ya Nigeria yakiri kutekwanyara kwa baadhi ya raia na Boko Haram
Serikali ya Nigeria imekiri kwamba
raia,wakiwemo watoto wametekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram katika
majuma ya hivi karibuni.
Msemaji Mike Omeri amesema kuwa ni vigumu
kukisia idadi ya watu ambao wametekwa wakati wapiganaji wa Boko Haram
wakitoroka wakati wa mashambulizi dhidi yao yanayotekelezwa na vikosi
vya kijeshi kutoka Nigeria,Chad na Niger.
Lakini msemaji wa
Nigeria alipinga madai kwamba zaidi ya watoto 500 walikuwa hawajulikani
waliko kutoka mji uliochukuliwa na jeshi Damasuk karibu na mpaka wa
Niger.
Nigeria imetangaza kwamba inafunga mpaka wake kuanzia siku ya jumatano usiku hadi jumapili huku uchaguzi wa urais ukifanywa.
CHANZO BBC.
Rais wa Iraq Fouad Massoum ametoa
ishara kwamba jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani huenda
likatekeleza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Islamic State mjini
Tikrit.
Katika kipindi cha siku chache zilizopita, muungano huo ulianza kufanya uchunguzi katika mji huo wa Iraq.
Bwana
Massoum ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba baada ya
kukusanya ripoti za uchunguzi wa ndege,muungano huo utaanza oparesheni
za kijeshi.
Hadi kufikia sasa ,Marekani imejiondoa katika jaribio la vikosi vya Kishia vya Iran kuuteka mji wa Tikrit.
Hatahivyo jaribio hilo limefeli huku mamia ya wapiganaji wa ISIS wakisalia katikati ya mji.
Rais wa Iraq hajasema iwapo serikali ilitaka mashambulizi ya angani ya Marekani katika mji wa Tikrit.
CHANZO BBC.
Robo ya wasudan Kusini wameathirika na njaa
Zaidi
ya watu milioni mbili unusu wanahitaji chakula cha msaada cha dharura,
baada ya kufurushwa makwao kutokana na mapigano kati ya jeshi la
serikali na vikosi vya waasi.
Mazungumzo ya kuleta amani yaliyokuwa yakiendelea katika taifa jirani la Ethiopia, yamesambaratika.
Haya
yanajiri siku moja tuu baada ya bunge kumuongeza rais Salva Kiir miaka
mitatu zaidi afisini na kuhairisha uchaguzi uliotarajiwa mwaka huu.
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anaelezea zaidi.
Hapa
ni katika mji wa Ganyiel kwenye jimbo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la
Unity, maelfu ya watu waliofurushwa makwao wamefika katika kituo cha
Shirika la WFP
ambapo wanapata mtama, mafuta na chumvi.
Kwa wengi hapa msaada huo ndio chakula cha pekee wakatachopata.
Shirika la WFP linasema mtu mmoja kati ya wane nchini humo, hawajui watapata wapi chakula
Nchi hii iliepuka kiangazi mwaka uliopita, lakini bado hakuna chakula cha kutosha. Asilimia kubwa ya raia wa Sudan Kusini wanahitaji chakula cha dharura
WFP inasema watu milioni mbili
unusu wanahitaji msaada wa dharura na idadi hiyo huenda ikaongezeka mara
mbili kufikia katikati ya mwaka huu, iwapo mapigano yataendelea.
Miongoni
mwa wanaopanga foleni hapa kutafuta chakula ni Elizaberth Nyalat
aliyetoroka mapigano katika mji wa Nyalat, Kusini Magharibi mwa Nchi
hiyo.
"nilikuwa nasomea mjini Yei, wakati vita vilipoanza.
Nilitoroka Yei hadi hapa.
Lakini sio kwa gari wala boti, nilikimbia kwa miguu.
Ilikuwa ngumu sana kwangu kufik amahali hapa."
Lakini
amani hiyo imekuwa ngumu kupatikana. Baada ya miezi kumi na mitano ya
mapigano yaliyofanya maeneo mengi kaskazini mwa nchi hiyo kuwa numu
kuyafikia.
Na sasa mashirika ya kutoa misaada yako mbioni kutoa
usaidizi kabla ya msimu wa mvua kuanza. Ertharin Cousin ni mkurugenzi
Mkuu wa WFP
"watu milioni tatu tunaojaribu kuwafikia,sio tu takwimu ni watu wa kweli. Asilimia kubwa ya raia wa Sudan Kusini wanahitaji chakula cha dharura
Tatizo ni kuwa , vita hivi
vinavyoendelea kwa muda mrefu, ndivyo watu hawa wanasahaulika na
kutazamiwa tu kama gharama au takwimu tu.
Lakini haya ni maisha ya watu. Ni binadamu."
Awamu
mpya ya mazungumzo ya amani yanatarajiwa kuanza tena mwezi
ujao...lakini huenda ikaathirika na hatua ya bunge hapo jana kumuongezea
Rais Kiir miaka mitatu zaidi mamlakani.
Uchaguzi wa mwezi Juni pia umeahirishwa.
Upinzani hata hivyo unasema hatua hiyo ya Kiir ni sawa na kukwamilia mamlaka.
Na huenda ikavuruga juhudi nzima ya kuleta amani nchini humo.
CHANZO BBC.
Injini ya treni ya mizigo ya kampuni ya Reli Tanzania, TRL
Marais wa Afrika Mashariki na kati
wamezindua rasmi mradi wa mabehewa mapya ya mizigo yatakayokuwa
yakisafirisha mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania
kwenda katika nchi za Rwanda, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi katika eneo hilo.
Uzinduzi
huo umefanyika Jumatano ambayo ni siku ya kwanza ya mkutano wa siku
mbili unaotarajiwa kuhudhuriwa na marais wote wa nchi hizo, hata hivyo
mpaka mkutano huo unaanza ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Pierre
Nkurunzinza wa Burundi pamoja na mwenyeji wao Rais Jakaya Kikwete ndio
waliokuwa wamehudhuria, huku Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame
wa Rwanda na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakituma
wawakilishi wao.
Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa nchi
hizo na wawakilishi wa mashirika na taasisi za fedha na wawekezaji
jijini Dar es Salaam, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema nchi yake
imedhamiria kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na nchi za eneo la ukanda
wa kati kwa kuboresha miundombinu ya barabara na reli na kupunguza kwa
kiasi kikubwa urasimu katika utoaji wa huduma za bandari na vikwazo vya
barabarani. Uzinduzi wa Treni ya Mizigo kwenda nchi za
Rwanda, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kutoka Dar es
Salaam, Tanzania.
Tatizo la uchelewashaji mizigo
katka bandari ya Dar es Salaam ni suala ambalo kwa muda mrefu limekuwa
likilalamikiwa na watumiaji wa bandari hiyo. Hata hivyo, sasa limeanza
kupatiwa ufumbuzi ambapo Katibu Mkuu wa wizara ya Uchukuzi nchini
Tanzania Dakta Shaban Mwijaka amesema muda wa utoaji wa mizigo katika
bandari ya Dar es Salaam umepungua kwa kiasi kikubwa kutoka siku 20 hadi
siku tatu, sababu kubwa akisema ni matumizi ya mfumo wa kielektroniki
badala ya kutumia makaratasi.
Nchi za Afrika mashariki na kati
zimepiga hatua katika uimarishaji wa miundombinu ya barabara, hata hivyo
rais Yoweri Museveni wa Uganda ameonya kwamba juhudi hizi hazitakuwa na
tija iwapo juhudi zaidi hazitafanyika katika kuboresha miundombinu ya
reli. Pia Rais Museveni amesema uvivu, rushwa na kutowajibika ni mambo
yanayokwamisha ustawi wa maisha ya watu wa kawaida katika eneo hilo na
Afrika kwa jumla.
Marais hao pia wamekagua miundombinu ya bandari,
na kuitaka mamlaka ya bandari ya Dar es Salaam kuongeza ufanisi zaidi
ili kuvutia wawekezaji katika sekta ya usafirishaji na miundombinu.
chanzo bbc.