Jumanne, 17 Machi 2015
TRAFIKI KUJA NA KANUNI KUWABANA MADEREVA WAZEMBE.
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Tanzania, kimeandaa kanuni na sheria kali dhidi ya madereva wazembe, ikiwa ni moja ya mikakati ya kukabiliana na wimbi la ongezeko la ajali za barabarani. Baadhi ya kanuni hizo ni pamoja na pendekezo linalompa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, mamlaka ya kuwalazimisha madereva wazembe, kwenda kozi ya mwaka mmoja katika vyuo vya mafunzo ya udereva, iwapo watabainika kuwa wamehusika kusababisha ajali za makusudi.
CHANZO EATV.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni