Jumanne, 17 Machi 2015
MAKINDA: BUNGE LINAMTAMBUA ZITTO KABWE KAMA MBUNGE
MH.ANNE MAKINDA.
Spika wa Bunge Mh Anne Makinda amesema kuwa kwa niaba ya Bunge bado anamtambua mbunge wa
Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuwa ni mbunge halali wa bunge hilo.
Akizungumza nje ya ukumbi wa bunge mara baada ya kikao cha Bunge kumalizika jana majira ya saa 5 Asubuhi, Makinda amesema kuwa anasubiri barua rasmi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo ndiyo itakayompa mwongozo kuhusu ubunge wa Zitto Kabwe.
Amesema kwa mujibu wa taratibu, kama chama kikimvua uanachama mbunge, kinapaswa kuiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo nayo inatoa mwongozo kwa bunge, jambo ambalo halijafanyika hadi sasa.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Mh. Tundu Lissu alipoulizwa kuhusu suala hilo amesema kuwa anayetakiwa kuandika barua hiyo ni Katibu Mkuu wa Chama, na si yeye na kwamba hajapata taarifa kama barua hiyo imeandikwa au la..!
Licha ya kuendelea kutambuliwa na uongozi wa Bunge, Zitto Kabwe leo hakuhudhuria kikao hicho cha Kwanza cha mkutano wa 19 wa bunge la 10.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni