Serikali ya Nigeria yakiri kutekwanyara kwa baadhi ya raia na Boko Haram
Serikali ya Nigeria imekiri kwamba
raia,wakiwemo watoto wametekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram katika
majuma ya hivi karibuni.
Msemaji Mike Omeri amesema kuwa ni vigumu
kukisia idadi ya watu ambao wametekwa wakati wapiganaji wa Boko Haram
wakitoroka wakati wa mashambulizi dhidi yao yanayotekelezwa na vikosi
vya kijeshi kutoka Nigeria,Chad na Niger.Lakini msemaji wa Nigeria alipinga madai kwamba zaidi ya watoto 500 walikuwa hawajulikani waliko kutoka mji uliochukuliwa na jeshi Damasuk karibu na mpaka wa Niger.
Nigeria imetangaza kwamba inafunga mpaka wake kuanzia siku ya jumatano usiku hadi jumapili huku uchaguzi wa urais ukifanywa.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni