Polisi wa mji wa Ferguson
Kamanda wa polisi katika mji wa
Ferguson nchini Marekani amejiuzulu baada ya ripoti ya shirikisho
kulaumu kitengo chake kina ubaguzi.
Thomas Jackson anakabiliwa na
miito ya kumtaka ajiuzulu tangu yalipotokea maafa ya kuuawa kwa kupigwa
risasi kwa Michael Brown, kijana mweusi ambaye hakuwa na silaha yoyote
wakati tukio hilo likitokea.Kijana huyo aliuawa na mmoja wa maafisa wake Agusti mwaka jana.
Meya wa eneo hilo James Jackson amemuelezea kamanda huyo wa polisi kama mtu muadilifu ambaye anatumai kuwa kuondoka kwake kutasaidia jamii kumaliza machafuko yaliyofuatia baada ya mauaji hayo.
Afisa wa ngazi za juu katika utawala wa mji wa Frguson na Jaji wa manispaa walijiuzulu mapema wiki hii.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni