Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumamosi, 21 Machi 2015

WATU 126 WAUAWA MSIKITINI YEMEN.

 
 Baadhi ya jamii za watu waliofariki ndani ya msikiti baada ya milipuko Yemen
Zaidi ya watu 126 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa, baada ya watu wa kujitolea muhanga kujilipua misikitini nchini Yemen.
Watu hao wameuwawa katika milipuko iliyolenga misikiti katika mji mkuu Sanaa wakati wa sala ya Ijumaa.

Milipuko Yemen
Waandishi Habari wanasema kuwa, misikiti yote miwili ni maeneo ya maombi kwa waislamu wengi ambao aaasi wa Ki-Shia, maarufu kwa jina Houthis, wanaodhibiti mji mkuu wa Sanaa.
Kwa miezi kadhaa sasa, kumeshuhudiwa taharuki kubwa kati ya makundi hasimu nchini Yemen, pamoja na makundi yaliyo na uaminifu na mtandao wa Al-Qaeda yaliyo katika maeneo ya kusini na mashariki mwa taifa hilo.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni