Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot
anasema kuwa hajakosana na meneja Arsene Wenger na kuongezea kwamba bado
hajaanza mazungumzo ya mkataba mpya na kilabu hiyo.
Mkataba wa Walcot unakamilika mwaka 2016 na Wenger amesema kuwa anatarajia kuwa na mda mrefu wa makubaliano.''Ripoti zinazosema nimekosana na kocha juu ya kandarasi ni upuzi mtupu'',alisema mchezaji huyo wa miaka 26.
Hatujaanza mazungumzo yoyote juu ya kandarasi yangu na lengo langu kuu ni kufanya vyema katika kilabu hii.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni