Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumamosi, 21 Machi 2015

IS YAKIRI KUSHAMBULIA MSIKITI YEMEN.

kundi la wapiganaji wa IS limekiri kutekelza ,mashambulizi katia misikiti ya Yemen 
Kundi la Islamic State linasema kuwa wapiganaji wake waliendesha mashambulizi ya kujitoa mhanga kwenye misikiti miwili nchini Yemen ambapo zaidi ya watu 130 waliuawa.
Washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walilenga waumini kwenye mji mkuu Sanaa wakati wa maombi ya Ijumaa.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na waumini wanaowaunga mkono waasi wa Shia wanaofahamika kama Houthi ambao walichukua udhibiti wa mji wa Sanaa mwaka uliopita.
Zaidi ya watu 200 walijeruhiwa wakati wa mashabulizi hayo ambapo wito wa kuwaomba watu kutoa damu umekuwa ukitolewa.
CHANZO BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni