Yanga ya Tanzania imeitumia salamu timu ya Platinum FC ya Zimbabwe kufuatia ushindi mfululizo katika ligi kuu ya Tanzania Bara.
Yanga
imeifunga JKT Ruvu 3-1 katika ligi kuu Tanzania Bara, huku Danny
Mrwanda, aliyewahi kucheza soka huko Vietnam akifunga goli moja na Simon
Msuva akitupia mawili katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Hivi karibuni, Yanga pia iliwafunga Mgambo Shooting 2-0 ikiwa ni
mfululizo wa ushindi katika mechi zakeMechi hizo ni sehemu ya maandalizi kwa safari ya Yanga kuelekea Zimbabwe kurudiana na Platinum FC katika mechi ya kombe la Shirikisho barani Afrika mapema mwezi ujao.
Yanga ilishinda 5-1 katika mechi ya awali ikiwa uwanja wa nyumbani na inahitaji ushindi wa aina yoyote, droo au hata ikifungwa magoli yasiyozidi 4 ili isonge mbele kunusa hatua ya 16 bora.
Yanga kwa sasa inaongoza ligi kuu Tanzania Bara ikiwa a pointi 40 katika michezo 19 iliyocheza huku Azam ikifuatia ikiwa na pointi 36 katika michezo 18 iliyocheza.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni