Mtoto anayonya maziwa ya mama
Utafiti uliofanyika nchini Brazil
umebaini kuwa watoto wanaonyonya kwa muda mrefu wanakuwa na akili
zaidi,wasomi,na wenye uwezo kifedha wanapokuwa watu wazima.
Ripoti
ya utafiti huo iliyochapishwa katika jarida la afya la Lancet Global
Health unafuatilia makuzi ya mtoto hadi kuikia utu uzima wake.Wataalam hao wanasema kwa mtoto anayenyonya kwa takriban mwaka mmoja anakuwa na kiwango cha akili cha juu zaidi ya yule ambaye hajanyonya kwa muda huo kwa kiwango cha IQ cha mara nne zaidi.
Katika maziwa ya mama kwa mjibu wa wataalam hao kuna madini mhimu ambayo husaidia ukuaji wa ubongo na kuongeza kiwango cha ufahamu.
Hata hivyo utafiti wa safari hii kwa mjibu wa wataalam hao nikwamba una uhakika zaidi kwani walitumia kubwa ya watoto tofauti na idadi iliyotumika awali miaka 1980.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni