Justice Joyce Aluoch kutoka Kenya kushoto
Majaji wa mahakama ya kimataifa
kuhusu uhalifu wa kivita ICC wamemchagua jaji wa Kenya Joyce Aluoch kama
makamu wa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kufuatia
uchaguzi huo uliofanywa siku ya jumatano,Jaji wa Argentina Silvia
Fernandez de Gurmendi alichaguliwa rais wa mahakama hiyo huku jaji
Kuniko Ozaki kutoka Japan akichaguliwa kama makamu wa rais wa pili.Urais wa Mahakama hiyo unawashirikisha rais na makamu wake wawili na unatoa mwongozo wa mahakama hiyo kwa jumla.
Rais wa ICC huwa mratibu wa mahakama hiyo na idara nyengine na hutoa mawaidha kwa kiongozi wa mashtaka kuhusu maswala yanayoleta wasiwasi kwa heshima ya mahakama hiyo.
Kulingana na mkataba wa Roma ,uongozi wa mahakama hiyo ya ICC ,unasimamiwa na rais huyo bila kumshirikisha kiongozi wa mashtaka.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni