Rais wa Yemen Abd Rabbuh Mansour Hadi
Rais wa Yemen aliyeko matatani, Abd
Rabbuh Mansour Hadi, ameliomba baraza la usalama la umoja wa mataifa
kuidhinisha hatua za kijeshi dhidi ya kundi la waasi la waislamu washia-
Houthi, lililomlazimu kuutoroka mji mkuu wa taifa hilo Sanaa.
Bwana Hadi tayari ameliomba baraza la mataifa ya muungano wa kiarabu kumsaidia kijeshi.Anajaribu kuunda makao mapya ya utawala katika mji wa bandari wa Aden Kusini mwa Yemen, lakini wanamgambo wa Houthi wameukaribia mji mkuu- Sanaa.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni