Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatatu, 23 Machi 2015

MVUA INAYOENDELEA KUNYESHA;HALI NI TETE JIJI LA DAR,

 
Hali tete inatawala katika jiji la Dar es Salaam kutokana na mvua ya masika inayoendelea kunyesha kwa siku nne mfululizo kusababisha vifo vya watu watano na nyumba nyingi zikiwa zimezingirwa na maji.
Maeneo yaliyoathirika zaidi mjini humo ni Buguruni kwa Mnyamani na eneo la Jangwani katika Manispaa ya Ilala, ambako nyumba nyingi na barabara zimeathirika.
Sehemu nyingine za jiji la Dar es Salaam zimezingirwa na maji kutokana na kuziba kwa mitaro na mifereji, ikiwa ni athari ya utupaji taka ovyo na pia miundombinu duni.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), mvua kubwa zaidi zinatarajia kuendelea kunyesha mpaka siku ya Jumatano.

Kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha, Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki jana aliongoza kikosi cha uokoaji katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani, ambako nyumba 250 zilizingirwa na maji, na vikosi vya uokoaji vimewanasua watu kadhaa waliokwama.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema kuwa, hadi kufikia jana mvua hizo zilikuwa zimesababisha vifo vya watu watano, akiwemo mtu mmoja aliyesombwa na maji, mwingine aliyeangukiwa na ukuta na watatu ambao walinaswa na umeme baada ya nguzo ya umeme.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni