Raia wa Sierra Leone waanza kusalia majumbani kwa siku tatu kwa lengo la kukabiliana na ebola
Mamlaka nchini Sierra Leone imeanza
kutekeleza hatua ya kutotoka kwa siku tatu miongoni mwa raia wake
itakayosaidia kukabiliana na kuenea kwa mlipuko wa ugonjwa wa ebola.
Takriban
watu millioni sita wametakiwa kusalia majumbani mwao kwa kipindi cha
siku tatu huku watu wa kujitolea wakitembelea nyumba hadi nyumba
kuwasaka watu walio na ishara za ugonjwa huo huku wakiwashauri wengine
jinsi ya kuepuka maambukizi.Visa kadhaa bado vinaendelea kuripotiwa kazkazini na Magharibi mwa Sierra Leone kila wiki.
Mataifa matatu ya Afrika Magharibi yalioathiriwa vibaya na Ebola Sierra Leone,Liberia,Guinea-yameweka lengo la kutokuwa na hata kisa kimoja cha ebola ifikiapo katikati ya mwezi ujao.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni