Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima
amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu
dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam,
Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.Akiongea kabla ya kuhojiwa na polisi Mchungaji Gwajima amejitetea kuwa alichofanya ni kutumia fursa ya kumuonya kiongozi mwenzake wa kiroho kutokana na kuwageuka wenzake katika makubaliano waliofikia katika tamko la kuipigia kura ya hapana Katiba inayopendekezwa.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kumkadhifu na kumtukana hadharani Kardinali
Pengo. Inadaiwa matusi hayo yameonekana kupitia mitandao mbalimbali ya
kijamii ya WhatsApp na mingineyo, ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na
picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana
kwa maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu
wengine.
CHANZO BBC.
CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni