Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 18 Machi 2015

WATALII 17 WA KIGENI WAUAWA TUNISIA

 
 Jengo la kumbukumbu la Tunisia lililolengwa na wapiganaji na kusababisha mauaji ya watu saba
Watu 19 wakiwemo watalii 17 wa kigeni wameuawa baada ya wapiganaji kulenga jengo moja la kumbukumbu za kihistoria katika mji mkuu wa taifa hilo amesema.Rais wa
Itali,Uhispania na Wajerumani ni miongoni mwa wale waliouawa waziri mkuu Habib Essid amesema.
washambuliaji wawili pamoja na afisa mmoja wa polisi wameuawa katika oparesheni ya kiusalama iliofanywa,maafisa wanasema.Shambulio hilo lilifanyika katika jengo la kumbukumbu la Bardo Museum ambalo liko jirani na bunge
katikati mwa Tunisia wakati wa shambulio hilo,wabunge walikuwa wakijadiliana kuhusu sheria dhidi ya ugaidi.
Watu wameondolewa katika majengo ya bunge.
Raia wa Uingereza,Italy,Ufaransa na Uhispania ni miongoni mwa waliotekwa wakati wa shambulizi hilo,kituo kimoja cha redio nchini humo kimetangaza.
Mateka waliosalia katika jumba hilo la kumbukumbu wameachiliwa ,shirika la habari la Reuters limesema baada ya kupata habari hizo kutoka kwa afisa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kutajwa.
chanzo bbc.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni