Timu ya Taifa ya Brazil itapepetana na Ufaransa katika mchezo wa kirafiki kwa mujibu wa kalenda ya Fifa.
Mchezo
huu wa miamba hawa wa soka utachezwa kwenye dimba la Stade de France,
Jijini Paris.Ni mchezo muhimu kwa timu zote, Ufaransa wanajianda na
michuano ya ulaya itakayofanyika nchini humo mwaka 2016.Huku Brazil
wakijiwinda na michuano ya Copa America. Mara ya mwisho timu hizi
kukutana ilikuwa mwaka 2013 ambapo Brazil waliichabanga Ufaransa kwa
mabao 3-0. mchezo huu utawakutanisha Didier Deschamps na Dunga makocha
waliokuwa manahodha wa timu zao wakati wa michuano ya kombe la dunia
mwaka 1998 Michezo mingine ya kirafika itakayopigwa hapo kesho ni pamoja
na Bahrain na Colombia,huku Chile wakipepetana na Iran.CHANZO BBC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni