Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 18 Machi 2015

MAMILIONI YA DOLA KUREJESHWA SWITZERLAND.

 
Hayati Sani Abacha,Rais wa zamani wa Nigeria
Serikali ya Switzerland inatarajiwa kurejesha kiasi cha dola za Kimarekani milioni 340 ambazo zilikuwa zimeibwa wakati wa miaka ya 1990 wakati Rais Sani Abacha akiwa kiongozi wa Nigeria.
Baada ya Bwana Abacha kufariki dunia mwaka 1998, Nigeria iliiomba Uswiss kusaidia kupatikana kwa zaidi ya dola bilioni mbili zilizokuwa zimehifadhiwa katika mabenki ya Ulaya na wana familia wa Rais Abacha.
Uswiss mwaka uliopita ilirejesha dola milioni mia saba kwa serikali ya Nigeria baada ya kumaliza mvutano wa kisheria.
Rushwa inabaki kuwa tatizo kubwa nchini Nigeria na katika mataifa ya nchi nyingi zinazoendelea hususan kutoka Afrika ambako wanasiasa mbalimbali wanatuhumiwa kujilimbikizia fedha katika mabenki ya Ulaya
CHANZO  BBC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni