Hali ya uharibifu nchini Syria
Ripoti ya mashirika zaidi ya
ishirini ya misaada ya kibinadamu na yale ya kutetea haki za binaadamu
yamelishutumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa
kutetea raia walio katikati ya vita nchini Syria.
Ripoti hiyo
imezishutumu nchi zenye nguvu kubwa ya ushawishi duniani kwa kushindwa
kutumia nguvu zao kuandaa maazimio ya kusaidia uhuru wa huduma za
misaada ya kibinadamu kwa waathirika.Ripoti ya masharika hayo ni ya kuadhimisha miaka minne ya vita nchini Syria ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa.
David Milband ambaye ni Rais wa Shirika la kimataifa la Uokoaji International Rescue Committee amesema kuna ongezeko dogo la misaada inayotolewa kuwasaidia raia wa Syria.
chanzo bbc
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni