wanajeshi wa ngazi za juu nchini Somalia wanachunguzwa kwa kushirikiana na kundi la wapiganaji wa Alshabaab
Mamlaka nchini Somalia imewakamata wanajeshi wake wa ngazi za juu na kuwatuhumu kwa kushirikiana na wapiganaji wa kundi la Al-shabaab.
Tayari maafisa 12 wanachunguzwa kwa madai ya kuwasaidia wapiganaji hao kushambulia hoteli ya The SYL katika mji mkuu wa Mogadishu mnamo mwezi Januari.
Ujumbe kutoka Uturuki ulikuwa ukiishi katika hoteli hiyo ukisubiri ziara ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Jeshi la serikali ya Somali linalosaidiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika linajaribu kulishinda kundi la Al-shabaab.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni