Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Alhamisi, 5 Machi 2015

HARUSI YA AINA YAKE MISRI.

 

Maharusi nchini Misri wameamua kufanya dhihaka kwa yanayoendelea Ulimwenguni na vitendo vya muuaji ambaye ni chinja chinja asiyeishiwa na kiu ya damu za watu wasio na hatia almaarufu ulimwenguni Jihad John ama Mohammed Emwazi,na wameamua kujitia kwenye tundu la chuma wakiwa na mwanamume anayepunga kisu hewani ikiwa ni namna ya mtindo wa kusherehekea harusi yao.
Harusi hiyo ya aina yake ilikuwa ikichukuliwa mkanda wa video,ilitukia eneo la Menoufia, nchini Misri huku mwanamume huyo apungaye jibisu hewani,uso ukiwa umevalishwa soksi maalum, akawaongoza wageni waalikwa kuingia shughulini, kisha akawaongoza maharusi kwenye kibweta cha chuma ama kisanduku basi kizimba itoshe hapo, sawa alivyowekwa yule rubani Mu'ath Al Kassasbeh wa nchi ya Jordan kisha akachomwa akiwa hai mwezi wa February si unakumbuka? Baasi ,mwenye jibisu mithili ya Jihad John akaamuru wimbo wa kijihad upigwe ambao ulitungwa na wanamgambo wa dola ya kiislam,ukapigwa.
Ndani ya hicho kizimba maharusi wapya wakaangusha densi ya nguvu kwa raha zao akiwemo mwanamume aliyeziba usowe, huku nje ya kizmba wageni waalikwa wakihanikiza kwa makofi na vigelegele kuwachagiza maharusi wajiachie na kufurahia siku yao muhimu maishani .
Wazo la kutafuta kizimba na hali ya kijihadi aliitoa bwana harusi,na alimtaarifu mkewe kuwa anamuandalia kitu tofauti kabisa na ndoa za watu wengine, akamtaka ajiandae kwa mshangao!
Ni bwana harusi pekee, wahudumu wa harusi hiyo akiwemo mpiga picha bwana , Ahmed Kassem, waloujua mpango huo kabla ya siku ya shughuli yenyewe.
Kabla ya kizimba kufunuliwa, wageni waalikwa walitaharuki wakiamini kuwa harusi imevamiwa na kundi la kigaidi la dola ya kiislamu IS, mashuhuda wanaeleza hivyo.
Lakini mwezi uliopita, zilioneshwa picha za mnato na za video zikionesha wa Misri wa madhehebu ya kikristo ya Coptic wakichinjwa na kundi hilo huko Libya.
CHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni