Kuchapishwa kwa kibonzo kwa mara nyingine kumeleta ghadhabu kwa jamii ya kiislamu
Serikali ya Ufaransa imewataka
waendesha mashtaka kuchukua hatua thabiti dhidi ya Watu waliotekeleza
vitendo vya kigaidi.Waziri wa Sheria nchini humo,Christiane Taubira
amesema maneno au vitendo vya chuki dhidi ya mwingine vinavyotolewa kwa
sababu ya imani ya dini vikomeshwe.
Zaidi ya Kesi 50 zimefunguliwa
dhidi ya Watu wanaotuhumiwa kuhusikana shambulio la kigaidi wiki
iliyopita na kusababisha watu 17 kupoteza maisha.Miongoni mwa walio matatani ni Said Koachi sambamba na shemejiye.Wakili wa Said ameiambia BBC kuwa Said alikuwa katika hali ya kawaida kabla ya shambulio kutokea.
Wakati hayo yakijiri,kumekuwa na mapokeo hasi kwa Waumini wa kiislamu baada ya kuchapishwa kwa Jarida lenye kibonzo kinachomuonyesha Mtume Mohamad akiomboleza.
Kiongozi mmoja wa kidini na Mufti wa Jerusalem ameita chapisho huwa kuwa ni tusi.Waziri wa mashauri ya kigeni wa Jordan,Nasser Joudeh amesema Charlie Hebdo kwa mara nyingine inapandikiza mbegu za chuki na migogoro.
Nako mjini Nouakchott, Polisi wamezuia maandamano ya Watu waliokuwa wakielekea Ubalozi wa Ufaransa, huku Mahakama ya Uturuki nayo ikipiga marufku kuchapishwa kwa Gazeti la Charlie Hebdo lenye kibonzo hicho.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni