Shule

Shule
Shule ya secondary Lilasia yenye usajili no. 3878 inatoa nafasi za kujiunga na kidato cha 1 mwaka 2015 shule ni ya kutwa na bweni. ofa! lipia kwa awamu nne. mawasiliano:- 0754 504 132/ 0756 240 471/ 0754 985 772 Wahi sasa nafasi ni chache

Jumatano, 14 Januari 2015

SIRI YA KASI BOLT YAFICHULIWA



Mwanariadha Usain Bolt 
Wanasayansi wanasema kwamba wanaweza kueleza kasi ya mwanariadha maarufu sana duniani Usain Bolt inatokana na nini kwa kutumia hisabati au hesabu.
Bolt alivunja rekodi kwa kumaliza mbio za mitya 100 kwa sekunde 9.58 wakati wa mashindano ya kimataifa mwaka 2009 mjini Berlin. Na hio ndio rekodi ya dunia.
Wanasayansi hao wanasema utafiti wao unafafanua kwamba nguvu na uwezo wa kimeili wa Bolt kuweza kustahimili upepo unasaidiwa na urefu wake wa futi 6 inchi 5.
Hata hivyo wanasanaysi hao wanasema bado wanafanya uchunguzi kujua kinachowafanya wanariadha wazuri kukimbia kwa kasi.
Kulingana na utyafiti wa wanasayansi hao waliotumia hesabu,kasi ya Bolt ya sekunde 9.58 mjini Berlin iliwezekana baada ya mwanariadha huyo kukimbia mita 12.2 kwa sekunde sawa na kasi ya mita 27 ka saa. .
Walisema kuwa Bolt alipata nguvu zake pindi alipoanza kukimbia chini ya sekunde moja na hiyo ilikuwa nusu tu ya kasi yake yote.
 Bolt baada ya kushinda mbio za dunia
Wanafizikia hao wanasema hii ina maanisha kuwa hapo ndipo hewa hupunguza nguvu zake za kusongesha vitu.
Pia walidungua kwamba chini ya asilimia nane ya nguvu za misuli yake ilitumika wakati alipokuwa anakimbia,
Rekodi ya Bolt mjini Berlin, ilikuwa nzuri zaidi kushuhudiwa tangu kuanza kutumika kwa kifaa cha elektroniki kuhesabu saa mwaka 1968.
''Ni vigumu sana kuvunja rekodi siku hizi, hata kwa sekunde moja kwani wanariadha wanahitajika kutumia nguvu nyingi sana dhidi ya upepo ambao huongezeka kwa kila ongezeko la kasi, '' walisema wanafizikia walofanya utafiti huo.
John Barrow wa chuo kiuu cha Cambridge alisema kwamba kasi ya Bolt pia ilitokana na ukubwa wa hatua zake za miguu licha ya kuanza mbio kwa kuchelewa.
"misuli yake inamsaidia sana kuongeza kasi licha ya kwamba mwenyewe ana kasi ya juu.''
Wanasema kwamba Bolt ana uwezo mkubwa wa kuvunja rekodi zaidi ikiwa ataanza mbio zake haraka na kwa kasi ikilinganishwa na mtindo waken wa sasaCHANZO BBC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni