Mtambo wa kuchimba Mafuta
Kampuni kubwa ya uzalishaji wa
mafuta Duniani ya Schlumberger imesema itapunguza ajira kwa kiwango cha
asilimia saba kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta ulimwenguni.
Wahudumu wa vituo vya Mafuta wakosa kazi
Hatua hiyo ya kupunguza
wafanyakazi inakuja kufuatia hali iliyotarajiwa ikiwemo matarajio kidogo
ya tofauti na gharama ya ugunduzi na uzalishaji wa mafuta kwa mwaka
2015. Makampuni tanzu ya mafuta ya Schlumberger yamepunguza ghrama za
uchimbaji mafuta kutokana na anguko hilo la bei. Bei ya mafuta katika
soko la Dunia imeanguka kwa zaidi ya asilimia 50 tangu mwezi June
mwakajana hali inayoathiri mataifa ambayo yamekuwa yakinufaika na
biashara za mafuta Duniani.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni